8 views 2 mins 0 comments

RC CHALAMILA  ATAKA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA KWA WANUFAIKA WA TASAF

In KITAIFA
March 12, 2025



-Asema ni muhimu kuelewa vizuri mfumo wa uboreshaji Kaya masikini  sambamba na taaluma ya ujasiriamali ili kuepuka kutumia pesa bila kuzalisha.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Machi 12, 2025 katika ukumbi wa mikutano Arnatoglo wakati akizindua zoezi la malipo ya Ruzuku kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini wanaoishi katika nyumba za kupanga kando ya barabara ya mabasi ya mwendo kasi (BRT)

RC Chalamila amesema uzinduzi wa malipo hayo kwa walengwa wa TASAF unalenga kusaidia wakazi wa mjini kunufaika na fursa za kiuchumi zinazoletwa na BRT kwa kupunguza gharama kubwa za kuishi pembeni ya njia za mabasi yaendayo haraka.

Mpango huu unasaidia Kaya masikini ambazo ziko katika hatari ya kushindwa kumudu kuishi karibu na njia ya BRT  kutokana na kuongezeka kwa gharama ya maisha kunakosababishwa na uwepo wa BRT na pia unalenga kusaidia wakazi wa mjini wenye kipato cha chini kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotokana na uboreshaji  wa usafiri kupitia mfumo wa mabasi yaendayo haraka.

Hata hivyo RC Chalamila baada ya kuwakabidi fedha wanufaika hao amewataka kuwa na matumizi sahihi ya fedha hizo, ” Ni lazima kuelewa mfumo mzima wa uboreshaji Kaya maskini sambamba na taaluma ya Ujasiriamali ili kuepuka kutumia pesa hizo bila kuzalisha, kwa mfano umeshapokea fedha unakwenda kufungua genge ili uzalishe zaidii ” Alisema  Chalamila.

Kwa upande wa TASAF wamesema katika hatua za kutatua changamoto  hizo mfuko wa maendeleo ya jamii  kupitia utekelezaji wa mpango  wa kunusuru Kaya masikini  wanoishi katika nyumba za kupanga kandokando ya barabara  ya mabasi yaendayo haraka, Fedha hizi ni kwa ajili ya kuwawezesha walengwa wa mpango wa TASAF kumudu gharama za maisha zilizopanda baada ya utekelezaji  wa ujenzi wa miundombinu ya DART

Mwisho uzinduzi huo umeudhuliwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila,  Wakuu wa Wilaya, Mameya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakurugenzi wa TANROAD na DART Menejimenti ya TASAF na wawekezaji wa mradi ngazi ya Halmashauri.

/ Published posts: 1805

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram