40 views 2 mins 0 comments

Tanzania Yajivunia Kujitegemea katika Ugavi wa Dawa za ARV, Hata Bila Msaada wa Marekani

In KITAIFA
March 02, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa amesema serikali ina hazina yakutosha ya dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi(ARVs) na kuwatoaย  hofu wananchi kuacha kuhifadhi dawa nyumbani.

Hayo yamebainishwa leo Machi 1,2025 Jiji Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga.

Amewataka na kusisitiza vijana kuwa makini na waangalifu na kujiepusha na tabia ovu zinazopelekea maambukizi ya magonjwa kama Ukimwi.

Aidha,amesemaย  ni muhimu kukumbuka kwamba Ukimwi bado upon na tumejipanga kupambana nao Ili kuutokomeza kabisa,pia amewatoa hofu na wasiwasi wale wanaotumia wataendelea kupata dawa hizo.

Serikali ya Tanzania imesema kuwa haitawaacha wananchi wake wapoteze maisha kutokana na ukosefu wa dawa za ARV, hata kama Rais wa Marekani, Donald Trump, atatekeleza mpango wake wa kusitisha misaada ya hisani kwa nchi za Afrika, ikiwemo dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi.

Msigwa, amesisitiza kwamba serikali imejidhatiti kwa kutenga fedha za kutosha ili kununua dawa hizo na kuendelea kuzitoa bure kwa wananchi wanaoishi na virusi vya HIV/AIDS.

“Serikali haitamuacha Mtanzania yeyote afe kwa kukosa matibabu,” amesema Msigwa. Amesisitiza kuwa kuna shehena ya kutosha ya dawa za ARV na kwamba wananchi wanaoishi na virusi vya HIV/AIDS hawapaswi kuwa na hofu, licha ya mabadiliko yanayoweza kutokea katika msaada wa kigeni.

Msigwa amewahimiza watumiaji Wa dawa hizo ambao hivi karibuni kutokana na hofu wamekuwa wakiomba kupewa dawa nyingi ili wahifadhi dawa kutokuhifadhi dawa kwa wingi, akisema kwamba dawa zinazozidi muda wake wa matumizi hupoteza ufanisi. Ameongeza kuwa serikali ina uwezo wa kugharamia dawa hizo kwa kutumia rasilimali zilizopo, na kwamba ukosefu wa misaada kutoka kwa nchi za Magharibi hakutaleta mtikisiko wowote wa kiuchumi nchini Tanzania.

Kauli hii imetolewa katika muktadha wa hofu inayozidi kuenea kuhusu athari za kutoshirikiana kwa karibu na Marekani, hasa kuhusu msaada wa dawa za ARV, ambapo baadhi ya wananchi walikuwa wakigombania na kuhifadhi dawa kwa wingi.

/ Published posts: 1816

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram