34 views 16 secs 0 comments

KAMERA 40 KUFUNGWA SOKO LA KARIAKOO

In BIASHARA
February 28, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

DAR ES SALAAM:

KATIBU Tawala mkoa wa Dar es Salaam Dk. Toba Nguvila amesema katika kuhakikisha usalama katika soko la Kariakoo, tayari serikali kupitia  Halmashauri ya jiji hilo imeshasaini mkataba na Wakalawa Ufundi  na Umeme  Tanzania  TAMESA kwaajili ya ufungaji wa kamera 40 za ulinzi ( CCTV Camera) kazi itakayoanza Machi Mosi mwaka huu zenye thamani ya  Shilingi milioni 514.

Amesema hii itasaidia katika kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.

Amesema Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) pia limeanza utaratibu wa kubadilisha nguzo za umeme kutoka za miti hadi za zege na kuweka nguzo za ili kuhakikisha linaboresha miundombinu ya umeme jambo ambalo limefikia asilimia 90 ya ukamilikaji  wake.

Amesema  pia  kwa kushirikiana  na Halmashauri  ya jiji, Wakala wa Barabara Vijijini ( TARURA), wanatarajia kufunga taa  730 katika  maeneo  ya Kariakoo  ili  kuhakikisha  mwanga  kwa masaa  yote  24.

Aidha ameninisha kuwa Jeshi la Polis pia limejipanga katika kuhakikisha usalama unakuwepo muda wote.

/ Published posts: 1818

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram