
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Taasisi ya Al- Madrasatul An-nujum imeandaa mashindano ya kuhifadhisha Quran Tukufu siku ya Tarehe 2 ya mwezi wa 3 2025 Katika ukumbi wa Dyccc chang’ombe jijini dar es salaam
Taasisi hiyo Mpaka Sasa imefikisha miaka 22 tokea kuazishwa kwake Kwa mashindano hayo ya kuhifadhisha Quran Tukufu Kwa vijana wadogo wa kiislam
Hayo Ameyasema Leo 24 Frebuari 2024 Balozi Masudi Kipanya na Ambae pia ni mshiriki atakae kuwepo siku hiyo Amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa siku ya jumapili ya ramadhan pili na mashindano hayo yataanza saa Moja kamili asubuhi na yatahusisha madrasa mbalimbali kutoka Tanzania
Kipanya Amesema mgeni rasmi wa siku hiyo atakuwa Mhe Ridhiwan kikwete waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na vijana na watu wenye ulemavu na mufti Shekhe Ally Namuruko na mkuu wa Wilaya ya temeke Dc mapunda na mkurugenzi wa Pbz bank na Rais wa yanga African Hersi kalia
“Mashindano hayo ni lengo la kuwaibua watoto b kumjua mungu wao pamoja na mtume wao kwani ndo kitu pekee ambacho kitakachowezesha kumjua mungu na kutenda mema hapa duniani”Amesema Kipanya
Nae supervisor wa hospital ya Royal Polyclinic Ally Msiro Amesema Tumekuwa watu wa karibu sana na madrasa ya An-nujum Kwa miaka 2 Sasa na sisi ni wadhamini wakuu Kwa upande wa Afya
Msiro Amesema kuwa siku hiyo watakuwepo kwa kuangalia hali ya kiusalama Kwa watu wote ambao watakaofika hapo na wamekuwa wakifanya chekapu Kwa wanafunzi wote Kwa awamu tofauti tofauti kwani wanahakikisha wanafunzi wanapokea maarifa yao wanakuwa Katika hali salama ya kiakili fikra na kimwili
“Mshindi wa kwanza atakaeshinda atapokea huduma ya matibabu bule ndani ya mwaka mmoja akiwa mzanzibar atapata huduma Zanzibar na akiwa dar es salaam atapata huduma hapa dar es salaam” Amesema Msiro
Pia Mwakilishi wa Kampuni za tiketi za ndege Khadija Ahmed Amesema kuwa sisi ni wadhamini wakuu Katika mashindano hayo na tunatoa zawadi Kwa mshiriki wa kwanza Kwa kumpeleka humla Katika mji wa Madina Kwa ajili ya kwenda kuhiji na kukaa ndani ya siku 2