49 views 49 secs 0 comments

RAIS MWINYI AFUNGUA TRACE AWARDS 2025

In BURUDANI
February 24, 2025



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema   Serikali itaendelea  kuwaunga Mkono  Wasanii kwani ni  Muhimu katika Kukuza Utalii, Uwekezaji na Urithi wa Utamaduni miongoni mwa Jamii.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipolifungua  Tamasha la Tuzo za Muziki la Trace Awards kwa mwaka 2025 linalofanyika  Hoteli ya The Mora ,Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja .

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Sanaa ya Muziki ina nguvu kubwa ya kuiunganisha jamii  na nyenzo muhimu ya kuchochea Ukuaji wa Uchumi , Uwekezaji na Ubunifu pamoja na kuibua Vipaji vya Vijana katika Sanaa.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ametoa rai kwa Waandaaji na Washiriki wa  Tamasha  hilo  mbali na Kufurahia Muziki bali pia litumike kujenga Ushirikiano, Umoja na  Mahusiano mazuri miongoni mwa Wasanii

Ameupongeza Uongozi wa Taasisi ya Trace Award kwa kuamua Tamasha hilo kufanyika Zanzibar kwa mara ya Kwanza kwani litaitangaza Zanzibar Kimataifa  pamoja na  Kukuza Utalii na kubainisha fursa za Uwekezaji na Utamaduni.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza  Wadau na Wafadhili mbalimbali kwa kufanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo na kuahidi kuwa Serikali kuendelea  kuweka Mazingira bora zaidi Kwa Wasanii na kazi za sanaa kwa lengo la Kukuza  Vipaji vya Vijana, fursa za Ajira na Urithi wa Utamaduni.

/ Published posts: 1905

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram