14 views 2 mins 0 comments

TAMTHILIA YA MILA NA UTAMADUNI YA ‘AFRICAN SPIRIT’ KUJA KUTANGAZA MAPINDUZI ZA MILA ZA AFRIKA

In BURUDANI
February 16, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Mkali Malela Herbalist Clinic Limited imeandaa tamthilia kubwa na ya kipekee inayoitwa “African Spirit” ambayo inayolenga kuibua na kuonyesha historia,Mila,na Utamaduni wa kiafrika Kwa kina.

Tamthilia hiyo ni nyenzo ya kuamsha fikra,kuonyesha thamani ya Mila za afrika na kuelimisha jamii Kuhusu umuhimu wa kuhifadhi urithi wa Africa Kupitia simulizi za kusisimua na maudhui yanayogusa.jamii na Tamthilia hiyo itakuwa Zaidi ya Burudani.

Ameyasema hayo Leo Tarehe 15 Frebuari 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Mkali Malela Herbalist Clinic Limited Riziki Mkali Malela wakati akizungumza na Mwandishi wa habari jijini dar es salaam Amesema Tunajivunia sana Kuanzisha mradi huu wa tamthilia Ya ‘African Spirit’

“Tunaamini kuwa tamthilia hii itakuwa chachu ya mabadiliko,SI TU Kwa kutangaza Mila na Utamaduni zetu,Bali pia Kwa kuelimisha na kuunganisha jamii ya afrika na ulimwengu mzima,”Amesema Malela

Aidha Malela Amesema kuwa Kuna mambo makuu yanayohusiana na Tamthilia hiyo ni kuonyesha Mila na desturi za kiafrika,ikiwemo sherehe za kitamaduni,Imani,za mizimu,na hekima za mababu zao

Pia Amesema kugusa matukio halisi ya maisha ya jamii za kiafrika,na jinsi tamaduni hizi zimeathirika na mabadiliko ya kisasa,kuleta ujumbe Kwa kizazi kipya,kuhamasisha kuthamini na kuhifadhi urithi wa afrika

Malela Ameelezea kuwa Tamthilia hiyo itakuza utambulisho wa kiafrika,Elimu na uhifadhi wa Mila na kuonganisha jamii

Pia Amesema Tamthilia hiyo itaandaliwa Kwa kutumia teknolojia za kisasa Ili kuhakikisha kuwa inakidhi viwango vya kimataifa na itahusisha wataalamu wa ndani na wa kimataifa Katika sekta ya  filamu.

/ Published posts: 1728

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram