13 views 4 mins 0 comments

WAZIRI MBARAWA AZINDUA MGAHAWA WA KFC STESHENI YA TRENI YA SGR JIJINI DAR ES SALAAM

In BIASHARA
February 11, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa Azindua mgahawa wa KFC uliopo Katika Stesheni ya Treni ya kisasa ya SGR jijini Dar es salaam Leo 11 February 2025.

Amesema kuwa Kwa Kufunguliwa Kwa mgahawa huu ni MATOKEO chanya ya Uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali yetu inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kufatilia Kwa kukamilika kwa miundombinu wa mradi wa SGR LUTA namba 1 na 2 na kuanza kutoa huduma za  USAFIRI na usafirishaji wa abiria kutoka morogoro mpaka dodoma



Ameyasema hayo Leo Tarehe 11 February 2025 Katika Stesheni ya Treni ya kisasa ya SGR jijini Dar es salaam akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya ilala Edward Mpogolo na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja kadogosa na Mmiliki wa Migahawa ya KFC

Amesema Tunamshukuru na kumpongeza Kwa dhati Mhe dkt SAMIA Suluhu Kwa kazi kubwa na nzuri ya Uwekezaji huu ambao watanzania tumeanza kuona matunda yake ikiwepo pamoja na fursa mbalimbali za ajira Katika majengo ya SGR kama tunaposhuhudia Leo

“Kwa kufunguliwa Kwa mgahawa huu wa kumi na Moja KFC Katika steshen ya sgr magufuri hapa  dar es salaam KFC imetoa fursa mpya za ajira Kwa watanzania hasa Kwa vijana Kampuni hii inaajiri na kutoa Mafunzo  Kwa watanzania Zaidi ya mia nane ikiwapa ujuzi muhimu Katika ukarimu,huduma ya Chakula,usalama wa Chakula,na usimamiZi Bora wa Chakula kwaniaba ya serikali tunakupongeza Sana Kwa kutayarisha ajira hizo”Amesema Mbarawa

Aidha Amesema Kupitia program zao za Mafunzo KFC hutoa fursa za ukuaji wa Muda mrefu Kwa wafanyakazi wao,wanakuwa na clear plan for development vestals Kwa vile hili pia ninawapongeza sana na hongereni sana




Pia Amesema kuwa Kwa UWEPO wa KFC Katika maeneo muhimu ya USAFIRI kama sgr unaimarisha shughuli za kiuchumi na kutoa ajira thabiti na fursa za kujenga ujuzi Kwa vijana Wetu wa kitanzania

“KFC inafanya shughuli za huhamasishaji wa matumizi ya bidhaa za ndani na ukuaji wa kiuchumi KFC inajitolea kuendesha mipango ya kuhamasisha  matumizi ya malighafi na vifaa vya ndani Kwa kuunga mkono wasambazaji wa wakitanzania.
“Na hili ni muhimu sana Kwa sababu hatutaki kuona Chakula kinachopikwa Katika migahawa yetu asilimia kubwa kinatoka nchi za nje Kwa hili tunawapongeza sana Kwa kazi nzuri mnayoifanya”Ameongeza Mbarawa

Halikadhalika Kampuni hii inafanya Kazi kwa ukaribu na  Kampuni za ndani Ili kuhakikisha bidhaa za kiwango Cha hali ya juu zinapatikana,ikiwa pamoja na kuku,mbogamboga,vifungashio na hivi karibuni wameanza KUTUMIA kechapu ambayo inayozalishwa na nyanya zetu Kupitia kiwanda kinachopatikana iringa kinachojulikana kama dabaga



Pia Waziri MBARAWA ametoa maelekezo kutoka Kwa TRC na KFC

Amesema Bado tunaamini kunafursa nyingi ya kazi yetu ya kwanza ni kutoa mazingira ambayo yanayovutia wawekezaji pia Bado tunaamini IPO fursa Kwa migahawa na vioski vya Chakula kuja kufanya kazi hapa, Bado IPO fursa” nendeni mkakae na watu wengine Ili biashara izidi na maduka ya vitu vidogo vidogo wasafiri mara nyingi huwa wanakumbuka mahitaji yao madogo madogo Kwa dakika za mwisho,Kwa mfano vinywaji dawa za haraka na vitu vidogo vidogo mukileta maduka hayo madogo madogo yataleta fursa hata kwetu sisi kama TRC pia italeta hamasa Kwa wasafiri Wetu”.


Pia ametoa maelekezo Kwa KFC Kwa kufungua tena  mgahawa dodoma kwani wasafiri wanaotoka dodoma ndo hao hao wanaotoka DAR ES SALAAM na morogoro


Wizara ya uchukuzi itaendelea kuunga mkono jitihada hizi za kuendeleza na kuboresha miundombinu na huduma za usafirishaji Kwa manufaa ya nchi yetu na nchi za jirani

/ Published posts: 1715

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram