6 views 2 mins 0 comments

BUNGE LAPITISHA TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII KUHUSU SHUGHULI ZA KAMATI KWA MWAKA 2024

In KITAIFA
February 08, 2025



Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeipitisha taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za kamati hiyo kwa kipindi cha Februari,2024 hadi Januari, 2025 huku likiitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya maboresho katika Sekta ya Maliasili na Utalii.

Akizungumza katika Mkutano wa 18, Kikao cha 9 cha Bunge hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya maboresho katika utaratibu wa makusanyo ya mapato kwenye taasisi za uhifadhi zilizo chini ya Wizara hiyo ili kurahisisha shughuli za uhifadhi ikiwemo ukarabati wa miundombinu ndani ya maeneo ya hifadhi.

Aidha, Mhe. Mnzava ameitaka Wizara hiyo kuendelea kugundua mazao mapya ya utalii sambamba na kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa njia ya kidijitali.

Kuhusu kuboresha huduma za malazi kwa watalii, Mhe. Mzava  ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya tathmini ya hoteli na lodges za Serikali zilizobinafsishwa kwa wawekezaji kwa lengo la kusimamia mapato na taratibu za uendeshaji wake.

Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema kuwa chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Sekta ya Utalii imekua ukilinganisha na kipindi cha kabla ya janga la Uviko 19.

โ€œTumefanikiwa kuongeza idadi ya watalii mpaka sasa tumefikia watalii milioni 5.3 na mapato yatokanayo na utalii yamefikia dola za kimarekani bilioni 3.6โ€ amesisitiza Mhe. Chana.

Mhe. Chana ameweka bayana kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu na huduma za malazi katika maeneo ya hifadhi na kwamba mpaka sasa Shirika la UNESCO limetoa  kibali cha kuridhia ujenzi wa barabara ya tabaka gumu kutoka Nabi hadi Fort Ikoma katika eneo la Ngorongoro.

Kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa dunia wa Ufugaji Nyuki (APIMONDIA) 2027 amefafanua kuwa mpaka sasa  limepatikana eneo lenye ukubwa wa ekari 48 kwa ajili ya mkutano huo na mchakato wa kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi unaendelea.

/ Published posts: 1709

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram