10 views 27 secs 0 comments

BWAWA LA KIDUNDA: SULUHISHO LA KUDUMU UPATIKANAJI WA MAJI DSM

In KITAIFA
February 06, 2025

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imethibitisha kuwa ujenzi wa Bwawa la Kidunda mkoani Morogoro umefikia hatua ya asilimia 27, huku mradi ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2026 kwa gharama ya shilingi bilioni 336.

Bwawa hili linajengwa kwenye mkondo wa Mto Ruvu na linatarajiwa kuhifadhi hadi lita milioni 190 za maji. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa uhakika, hasa wakati wa ukame katika maeneo yanayopata huduma kupitia mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.

Katika ziara ya waandishi wa habari na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mnamo Februari 6, 2025, Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mkama Bwire, alieleza kuwa bwawa hili halitasaidia tu kupunguza uhaba wa maji bali pia kudhibiti mafuriko na kuzalisha megawati 20 za umeme zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Mbali na kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama, mradi huu unatarajiwa kuchangia maendeleo ya viwanda, kilimo, na kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla. Serikali imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuimarisha huduma za maji na nishati kupitia miradi mikubwa kama Bwawa la Kidunda.

/ Published posts: 1703

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram