14 views 51 secs 0 comments

WAZIRI MBARAWA AITAKA TRC KUHAKIKISHA MRADI WA UVINZA-MUSONGATI KUKAMILIKA KWA WAKATI

In BIASHARA
January 31, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amelitaka Shirika la Reli Tanzania(TRC) kuhakikisha mradi wa reli ya Uvinza-Musongati unakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji baina ya Tanzania, Burundi na DRC.

Ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa kipande cha saba na nane cha Uvinza(Tanzania) – Musongati(Burundi) kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na ubia wa kampuni za China Railway No. 2 Engineering Group Co. LTD na China Railway Engineering Design and Consulting Group Co. LTD.



Waziri Prof Mbarawa amesema mradi huo utakaogharimu Tsh. trillion 5.6 fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) utekelezaji kwa miezi 72 ikijumuisha na muda wa matazamio wa miezi 12.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemtaka Mkandarasi Kampuni ya wa kampuni za China Railway No. 2 Engineering Group Co. LTD na China Railway Engineering Design and Consulting Group Co. LTD kuhakikisha anakamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa.



Kwa upande wake Waziri Wa Miundombinu, Ardhi na Makazi wa Burundi Nahodha Dieudonne Dukundane amesema kuanza kwa utekelezaji wa mradi kunaongeza kasi kwa Nchi hiyo kukamilisha usanifu kwa sehemu iliyobaki itakayounganisha reli hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)

Naye Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amewahakikishia wadau wa uchukuzi kuwa fedha zipo na hakuna mradi utakaokwama kwa kukosa fedha.

/ Published posts: 1695

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram