8 views 18 secs 0 comments

WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.

In KITAIFA
January 31, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema Chama na serikali yake haitakubaliana na azimio lolote litakalotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kukutana kwa faragha kama walivyotangaza viongozi wa chama hicho, juzi.

Amesema amesikia chama hicho kikitangaza kwamba kinakwenda kujifungia kisha kije na jambo ambalo halijapata kushuhudiwa nchini, hivyo ametoa angalizo jambo hilo ni lazima lifuate sharia za nchi.

Wasira amesema hayo leo alipohutubia wananchi katika mkutano uliotumika kuzindua sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi ya Zamani mjini Bunda.

โ€œWamesema wanajifungia halafu waje wafanye jambo ambalo halijapata kuonekana, nikasema ni jambo gani, mimi nikaona huko kujifungia ile ni honeymoon maana honeymoon simnaijua, watu wakishaoana wanajifungia mahaliโ€ฆile ni honemoon.

โ€œTunawaambia tunawatakia heri kwenye honeymoon lakini tunawaambia lolote watakalotoka nalo kwenye honeymoon lazima lifuate sheria, waklija na honeymoon inavunja amani hatuwezi kuwaunga mkono.

/ Published posts: 1689

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram