51 views 44 secs 0 comments

WAWILI WAKAMATWA KUHUSIANA NA TAARIFA YA RAIA WA KIGENI KUTEKWA NA KUPIGWA.

In KITAIFA
January 25, 2025



Na. Mwandishi Jeshi la Polisi Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watuhumiwa wawili kuhusiana na taarifa inayosambaa katika mtandao wa kijamii ikieleza kunusurika kuuawa, kutekwa na kupigwa nyundo kichwani kwa raia mmoja wa kigeni aitwaye Suzan Mary Shawe (75) raia wa afrika kusini.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo amesema kuwa tarehe 21.01.2025 muda wa 03:00 asubuhi huko maeneo ya njiro Block C1 katika halmashauri ya jiji la Arusha Suzan Mary Shawe alishambuliwa na watu waliotumwa na wakili Qamara Valerian (36) ambaye ni wakili wa kujitegemea kwa nia ya kumtoa kwa nguvu kwa madai ya kuto lipa kodi ya nyumba.

SACP Masejo ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia watuhumiwa wawili katika tukio hilo la kumshambulia raia huyo wa kigeni ambao ni Qamara Valerian (36) ambaye ni wakili wa kujitegemea na Benjamin Paul (19) dereva pikipiki (bodaboda).

Vilevile amefafanua kuwa Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na mara baada ya upelelezi kukamilika taratibu nyingine za kisheria zitafuata.

Pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha likasisitiza kufuatwa kwa sheria na kanuni katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.

Sambamba na hilo limetoa rai kwa baadhi ya waandishi wahabari kufanya uchunguzi wa taarifa zao na kujiridhisha kabla ya kuzitoa ili kuondoa taharuki kwa wananchi na wageni wanaofika katika Mkoa wetu.

/ Published posts: 1744

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram