
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 29, 2024 huku matokeo ya wanafunzi 67 wakiwemo watano walioandika matusi yakifutwa.
Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi Januari 23, 2025 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohammed jijini Dar es Salaam. Amesema wanafunzi hao wameandika matusi ni tatizo la maadili. “Maadili, matusi hayakubaliki chumba cha mtiani na kila mahali, mwaka huu wametokea wanafunzi watano wameandika matusi,” amesema Dk Mohammed.
Baraza la Mitihani la Tanzania, limewafutia matokeo ya Kidato cha nne wanafunzi 67, waliogundulika kufanya udanganyifu pamoja na watano kwa kuandika matusi kwenye majibu ya mtihani waliofanya wa kuhitimu Elimu ya sekondari.
Aidha Baraza limezuia matokeo ya wanafunzi 459 kwa sababu za kiafya zilizopelekea kushindwa kufanya mtihani wa Kidato cha nne 2024