25 views 53 secs 0 comments

TEF YAWAPONGEZA SAMIA,DKT MWINYI,DKT NCHIMBI

In KITAIFA
January 21, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-DAR ES SALAAM

MKUTANO Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Dodoma Januari 18 na19, mwaka huu umewateua Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwamgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwamgombea mwenza (Makamu wa Rais) wa Dkt. Samia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huuwa2025.

Pia mkutano huo umemchagua Stephen Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCMTanzania Bara.

“Sisi Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) tunawapongeza viongozi hawa walioteuliwa na kuchaguliwakwa nyadhifa hizi. Matumaini yetu kama Jukwaa ni kuwa viongozi hawa wataendeleza jukumula kulitumikia taifa la Tanzania na kuwakomboa wananchi kutoka katika lindi la umaskini nakuwaletea maendeleo ya kweli.

“Tunaamini viongozi hawa watakapopata nafasi kwa maanayakuchaguliwa wataendeleza utamaduni na jukumu la kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombovya habari bila vikwazo vya aina yoyote,” alisema Balile katika taarifa yake kwa umma.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa kama alivyosema Rais Samia kuwa uhuru wa vyombo vya habari umeongezeka nchini, tunatamani nchi yetu itanue wigo wa uhuru wa vyombo vya habari wananchi wapate kilataarifakwa wakati ziwasaidie kufanya uamuzi wakiwa na taarifa sahihi.

“Hongereni sana mlioteuliwa kwa nyadhifa hizo, tunatumaini Watanzania wakiwachaguakatikauchaguzi mkuu wa mwaka huu, mtaendeleza misingi imara ya nchi hii ya amani, upendo, utulivu, mshikamano na Muungano wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania,” alisema

/ Published posts: 1695

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram