Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, amesema kuwa serikali inajizatiti kutatua changamoto zinazotokana na mvua katika usafiri wa treni za Mwendokasi (SGR). Kadogosa ameeleza kuwa mvua kubwa inayoendelea kunyesha inasababisha maji kuingia katika sehemu ambazo ziliharibiwa na wahalifu, hivyo kusababisha hitilafu katika miundombinu hali iliyopelekea kusimamisha kwa treni kwa masaa 6 hadi 7 njiani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kadogosa amesemakuwa serikali imejipanga kurekebisha maeneo yote yenye changamoto ili kuhakikisha usafiri wa treni unakuwa salama na haukwami njiani huku akishukuru Jeshi la Wananchi kwa kudhibiti wizi wa mitambo ya reli na kusema kuwa sasa hali ya usalama imeimarika.
Kadogosa aliongeza kuwa idadi ya abiria wanaosafiri kwa treni ya SGR imeongezeka, ambapo takribani watu milioni 1.4 wamesafiri katika kipindi cha miezi minne, na kila siku watu kati ya 5,000 hadi 10,000 hutumia treni za Mwendokasi.
Aidha Kadogosa amethibitisha kuwa Shirika la reli nchini Tanzania TRC kwa kushirikiana na jeshi la polisi linaendelea Kudhibiti uhalifu wa miundombinu ya reli ya kisasa na Changamoto Zinazotokana na mvua kwenye miundombinu ya usafiri Wa treni hiyo.
amesema kuwa Kutokana na changamoto zilizojitokeza katika shirika letu kwa sasa vitendo vya uhalifu vimepungua kwa kiasi kikubwa zaidi hivyo tunaenda kumaliza changamoto hiyo katika usafiri wa treni za Mwendokasi (SGR).
“Nitoe pongezi kwa serikali kuweza kutumia usafiri wetu wa treni kwani zaidi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi CCM, Wasanii mbalimbali na viongozi wa chama hicho kutoka Zanzibar, Lindi, na Mtwara lengo ikiwa ni kwenda kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kwenda kufanyika mkoani Dodoma tarehe 17,18.
Aidha Kadogosa ameongeza kuwa kipindi cha mvua zinazonyesha inapelekea maji kuingia katika sehemu ambazo ziliharibiwa na wahalifu, hivyo kusababisha hitilafu ya miundombinu kusimama kwa treni kwa masaa 6 hadi 7 njiani” Amesema Mkurugenzi kadogosa.
Vilevile Tunaendelea kutatua changamoto kwenye maeneo ya miundombinu ili kwenda kuhakikisha usafiri wa treni unakuwa salama zaidi kwa abiria wote.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya kisarawe Mhe.Petro Magoti ametoa pongezi kwa serikali kwa kuweza kutumia usafiri wa treni hiyo kuelekea kwenye mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika mkoani dodoma mwaka huu.
Takribani ya wajumbe ambao wanaelekea kwenye mkutano huo na wasanii ni chachu ya kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi katika kutumia usafiri huo pia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anahakikisha wananchi wake wanatumia usafiri huo wa haraka.