16 views 4 mins 0 comments

TUCTA YATOA MUSWADA YA MAMBO 9 KATIKA SHERIA ZA KAZI NCHINI

In KITAIFA
January 16, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) likiwa ndiyo mwakilishi wa wafanyakazi Tanzania na moja wa wadau wakubwa wa sheria za kazi Nchini, tulipokea mapendekezo ya marekebisho ambayo tayari yamekua ni mswada na baadae tukapokea mwaliko wa kuwasilisha maoni yetu kama wadau.

Yafuatayo ni baadhi ya maeneo ambayo tumeyatolea maoni ambayo tuna imani yatakua na matokeo  chanya kwa wafanyakazi Tanzania.

1. Muswada unapendekeza kuondoa neno Sunday kwenye tafsiri inayohusu basic wage.  Sisi kama wawakilishi wa wafanyakazi tumeona neno hilo libaki kwa sababu ni utamaduni wetu wa muda mrefu  na hivyo kama kuna haja ya kuongeza neno jipya la rest day  basi liongezeke bila kuathiri neno Sunday.

2. Muswada pia unapendekeza kuongeza wigo wa tafsiri wa neno  senior management employee kwa kujumuisha wafanyakazi wenye mamlaka ya kuajiri, kinidhamu na kusitisha ajira nao kutambulika kama senior management empoyee  . Kwa upande wetu kama TUCTA tumeshauri kamati maana ile ibaki kama ilivyokua kwa sababu wafanyakazi wengi watajikuta wanaangukia kwenye kada hiyo ya senior manangement employee na kusababisha kukosa haki zao za msingi ikiwemo malipo ya masaa ya ziada na kujumuika kupitia vyama vya wafanyakazi kama ilivyo katika sheria ya sasa. Kwa Mfano dereva anayewajibika moja kwa moja kwa msimamizi (supervisor) kutambulika kuwa senior management employee.


3. TUCTA pia tumependekeza kuwa mfanyakazi anayejiriwa kwa misingi ya kupata mafunzo (trainee) afanye mafunzo hayo kwa kipindi cha miezi isiyozidi 12 tu kisha aajiriwe kama mfanyakazi kamili badala ya miezi 24 iliyopendekezwa na muswada.

4. Muswada unapendekeza kwenye maswala ya dharura/majanga mwajiri akae na mfanyakazi kukubaliana namna ya kushughulikia hilo suala. Maoni ya TUCTA ni kuwa pale amabapo kuna chama cha wafanyakazi mwajiri ashauriane na chama hicho ili kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi. Mfano hatma ya ajira na ujira kwa mfanyakazi.

5. TUCTA tumependekeza pia iwapo mama atajifungua mtoto kabla ya muda wa kujifungua haujatimia (mtoto njiti) basi mama apewe muda wa uangalizi wa mtoto mpaka mtoto akamilishe wiki 40 badala ya wiki 36 zilizopendekewa na muswada, kisha mama apewe likizo ya uzazi ambayo haitaathiri ule muda wa uangalizi mtoto kabla ya kukamilisha wiki 40.

6. TUCTA tunapendekeza pia likizo ya dharura ambayo haitakua na malipo kwa mfanyakazi mwenye uhitaji iwe angalau miaka 5 ili kukidhi mahitaji ambayo huenda yakawa ni ya kiuongozi ama kimasomo badala ya siku 30 iliyopendekezwa na muswada.


7. TUCTA tunashauri pia nafuu ya mtu anasitishiwa ajira kwa kutokufuata taratibu au kutokuwepo na sababu zenye mashiko basi alipwe fidia/nafuu ya mishahara kulingana na sheria iliyopo sasa tofauti na mapendekezo ya muswada ambayo yameweka ukomo wa mishahara isiyozidi miezi 12. Mapendekezo ya muswada uliopo sasa yatasababisha uwepo wa fidia zisizo na uhalisia na pia kuwapa mamlaka waajiri kusitisha ajira za wafanyakazi pasipo kufuata utaratibu. Lakini pia itaondoa maana ya uwepo wa kanuni za utendaji bora tangazo la serikali namba 42 la mwaka 2007 (code of good practice). TUCTA inashauri vyombo vyetu vya utatuzi wa migogoro ya kikazi nchini vimekuwa vikifanya kazi yake kwa umahiri mkubwa kwa kutoa fidia zinazostahiki kwa kuzingatia sheria iliyopo sasa.

8. TUCTA pia imependekeza kuwa, wakati wa majadiliano ya mkataba wa hali bora za kazi,katika taasisi za umma , endapo mkataba utapelekwa kwa Katibu Mkuu kwenye wizara husika, mkataba huo uutolewe maamuzi na Katibu Mkuu kwenye wizara husika ndani ya siku 60 badala ya kutokuwa na ukomo wa muda wa kimaamuzi katika muswada wa sasa.

9. TUCTA imeendelea kupendekeza kuwa chama cha wafanyakazi chenye mamlaka ya kujadiliana na mwajiri wakati wa  kuunda mabaraza ya wafanyakazi kiwe ni kile chama  kinachotambulika na mwajiri kama ilivyo kwenye sheria ya sasa na chama kilichosajiliwa na kina wanachama katika eneo hilo.
Ndugu Wanahabari,
Ni Imani yetu kuwa mapendekezo haya yamepokelewa na yatakubaliwa kwa maslahi mapana ya wafanyakazi wa Tanzania.

/ Published posts: 1642

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram