24 views 4 mins 0 comments

KITUO CHA GESI YA SNG CHA UBUNGO KUAZA KUJAZA GESI FEBRUARI 2

In BIASHARA
January 09, 2025

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko, amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo kikuu cha kushindilia gesi asilia (CNG) kilichopo Ubungo, Dar es Salaam. Ametangaza kuwa kituo hicho, kinachojengwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kitaanza kutoa huduma za kujaza gesi asilia kwenye magari kuanzia Februari 3, 2025.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dotto Biteko wakati wa ziara ya kutembelea kituo cha kujaza gesi kituo kinajengwa shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Amesema mitambo yote inayohitajika imeshawasili na Ujenzi utakamilika ndani ya wiki moja umekamilika na maandalizi yamekamilika.


“Mkandarasi ametuhakikishia itakapofika Februari 03, 2025ย  kwa mara ya kwanza magari yatakuwa yanakuja kujaza gesi hapa.” Amesema Dkt. Biteko

Amesema malengo ni kuondoa foleni ambazo zinajitokeza katika vituo vya kujazia gesi katika magari, Pikipiki na Bajaji..

Amesema mwitikio wa Watanzania kuhama kwenye matumizi ya mafuta kwenda kwenye nishati safi umekuwa mkubwa sana ndio maana watu wanaotumia vyombo vya usafirishaji wanatumia gesi asilia.

“Na serikali Rais Samia ameshatoa maelekezo tujenge vituo vingi zaidi katika jiji la Dar es Salaam ambako ndio mtumiaji mkubwa wa gesi.”

Amesema kutajengwa kituo kingine cha kujazia gesi asilia katika vyombo ya usafiri, lakini wakati huo huo kunavituoย  vingine saba vinajengwa na sekta binafsi.


Amesema nia ni kuona kwamba vituo hivyo vinaongezeka idadi mpaka kufikia vituo 15, wakati huo huo kuwe na vituo vinavyotembea ambavyo vitakuwa morogoro kimoja na Dodoma vitakuwepo viwili.


“Nataka tuwahamishe sananchi kutoka kwenye matumizi ya nishati siyokuwa safi kwenda kwenye nishati safi ambayo Rais Samia ni Kinara wa Nishati safi Afrika na hasa nishati ya kupikia.”

Amesema kuwa watahakikisha kuwa vituo hivyo vinajengwa kwa haraka, pia amewapongeza TPDC kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuajiri vijana wakitanzania kwaajili ya kusaidia kazi za ujenzi wa kituo hicho.


Bilioni 18.9 zinatumika kufanya kazi ya ujenzi wa kituo cha kujazia gesi asilia cha Samnujoma, mhimbili pamoja na Kairuki vyote hivyo ni fedha kutoka TPDC.

Akizungumzia matumaini ya ujenzi wa kituo cha gesi asilia kwaajili ya kujaza kwenye vyombo vya usafiri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema matumaini ni makubwa kwani februari 03,2025 magari yataana kujaza gesi katika kituo hicho.

Amesema kituo hicho ni kituo mojawapo kilichopo katika mipango ya maendeleo kabla ya kuisha mwaka wa fedha wanatagemea kuwe na vituo vingine saba ambavyo vitakuwa Mbezi Beach, Tegeta, Mwenge, Simu 2000, Muhimbili na kibaha ikiwa na nia ya kuwawezesha wananchi wanaotaka kubadilisha magari yao kutumia gesi au wameshabadilisha waweze kuwa na nishati safi ya gesi katika magari yao.

Amesema mipango ya wizara kwenye eneo la gesi asilia linakwrnda vizuri hasa kwenye matumizi ya kawaida.

Licha ya hayo, Mhandisi Mramba amesema wamekubaliana naย  Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kwamba magari yatayokuja yatakuwa na uwezo wa kutumia gesi asilia.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Profesa William Anangisye amesema kuwa ujenzi wa kituo cha SNG katika eneo la UDSM utawanufanisha hasa katika kutoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi wa chuo hicho pamoja na fursa mbalimbali zitakazojitokeza kwa wanafunzi wanaosomea masuala ya gesi.

Pia amesema kuwa watahakikisha kituo hicho kipo salama muda wote kutokana na kuwa katika eneo hilo. Na ajira nyingi zitakazopatikana zitasaidia vijana wa kitanzania.

/ Published posts: 1633

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram