Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Katibu Tawala wa mkoa wa dar es salaam Toba nguvila Amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya ubungo waanze mkakati wa haraka sana wa ujenzi wa uzio wa hospital Kwa kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya uzio
Ameyasema hayo Leo Katika Kuendelea na ziara yake ikiwa ni siku ya pili Kwa kutembelea Halmashauri zote za mikoa ya dar es salaam
Amesema hapa Kuna wagonjwa na wanaitaji usiri na utulivu,kunapokuwa na mwingiliano wa watu wengi zile Siri za ugonjwa zinakuwa hadharani na jambo la uzio halikwepeki na kuwataka ujenzi uaze mara Moja Ili kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapata huduma Bora na salama Katika mazingira mazuri
Aidha Nguvila Amemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuongeza watumishi Katika hospital hiyo ya Wilaya Amesema vizuri Kuna watendaji wazuri sana ambao walioletwa hapa,sambamba na maboreshaji wa mazingira haya,na kuwataka waongeze idadi ya watumishi na idadi ya wagonjwa ni wengi sana na watumishi waliopo hapa ni wachache na haikudhi haja na hoja ya kuwa na hospital ya Wilaya
Halikadhalika Ameongeza kuwa majengo yaliyokuwepo haijafikia Ile level ambayo serikali wanayoitaka kwenye hadhi ya hospital ya Wilaya,Bali huduma inatolewa kama za hospital ya Wilaya lakini majengo haijafikia hadhi Ile
“Tumieni Bajeti zetu zile za makusanyo mnayo yakusanya Kwa kuongeza baadhi ya majengo ila Kwa yale yanayoitajika kuombwa munaitajika mufate utaratibu wa Bajeti na kuweka Katika Bajeti kuu Ili tupitishe mikoani iende tamisemi na badae iende bungeni Kwa kuidhinishwa”. Amesema Nguvila
Mkuu wa Idara ya lishe na jamii na Mganga mkuu wa Manspaa hospital ya Wilaya ya ubungoTwelitweli mwinuka Amesema Hospital ya Wilaya ya ubungo inachangamoto mbili ambazo zinaitajika kutatuliwa na serikali
Amesema Hospital kutokuwa na uzio kunapelekea usalama wa hospital na mali zake kuwa mdogo,na kutokuwa na walk way na kupelekea changamoto ya kuwahudumia wagonjwa wasioweza kutembea wenyewe hasa kipindi Cha kuwahudumia kutoka jengo Moja kwenda jingine kupata huduma ya vipimo na kulazwa.