Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA y
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ina Mchango Mkubwa katika Mipango na Sera za kuendeleza Uchumi wa Buluu unaozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi Jengo la Taaluma na Utawala la taasisi hiyo Buyu ,Wilaya ya Magharibi B ,Mkoa wa Mjini Magahribi.
Aidha Rais Mwinyi ameahidi Serikali kuendelea Kushirikiana na Taasisi hiyo wakati wote kwa lengo la kuhakikisha Rasilimali za Bahari ziliyopo zinatumika ipasavyo ili kutoa Mchango Mkubwa kwa Uchumi na Ustawi wa jamii.
Amefahamisha kuwa kuimarika kwa Miundombinu ya Taasisi hiyo hapa Zanzibar kutatoa mchango mkubwa wa sekta nyengine muhimu ziliyomo katika Uchumi wa Bulu .
Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa matarajio ya Serikali ni kuona Sekta ya Utalii inayochangia asilimia 30 ya Uchumi wa nchi ,Uvuvi ,Ukulima wa Mwani na Mazao ya Baharini zinaimarika kupitia Tafiti zitakazoandaliwa na Taasisi hiyo pamoja kutoa Wataalamu wenye weledi watakaojifunza katika taasis hiyo.
Amezitaja sekta nyengine kuwa ni Bandari, Mafuta na Gesi na Usafiri wa Baharini.
Ameyalezea Matarajio mengine kuwa ni kwa Taasisi hiyo Kufanya Tafiti za Uchumi wa Buluu zitakazotoa Matokeo bora kwa ajili ya Uandaaji wa Sera na Mipango ya Maendeleo ya Sekta hiyo.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ametumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia kwa Mchango wao katika miradi mingi ya Maendeleo nchini kitendo kinachoonesha Kuaminika kwa Serikali zote mbili za SMT na SMZ kutokana na Matumizi mazuri ya fedha za Miradi ya Maenďeleo na Kuwasisitiza kuendelea na Mchango huo.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ametoa rai kwa Wawekezaji kulitumia Eneo la Buyu kuchangamkia Fursa za Uwekezaji kutokana na Mandhari nzuri ya eneo hilo kwa Makaazi na Malazi kwa Wanafunzi ,Huduma za Usafiri ,Kumbi za Mikutano ,Huduma za Utafiti ,Hospitali , Utafiti wa Bahari na Shughuli mbalimbali za Kijamii.