Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Kitabu hiki nimeandika niweze kusaidia watu wengi japo watu wengi ni wavivu kusoma nataka niwakumbushe kwamba ufalme utatekwa na wenye nguvu lazima tulipe gharama ili tuweze kuishi hatma yetu tulopewa na Mungu.
Hayo ameyazungumza Mbeba maono Mchungaji Gabriel Hassan katika hafla ya uzinduzi wa kitabu chake cha Nguvu ya utendaji wa madhabahu ambacho amekiandika ili kuweza kuwakomboa watu na madhabahu za ukoo ambazo ni tatizo linalowasumbua watu wengi toka enzi na enzi.
“Maono ya kuandika kitabu hiki yalitokana na somi ambalo nilikuwa nafundisha nikienda kuhubiri injili sababu madhabahu ina nguvu kubwa katika maisha ya mtu hata ukoo ambapo zile roho za ukoo zinatembea na watu kila mahala hivyo kila familia zina shida za ukoo jitahidi kupata nakala yako uweze kupata uponyaji “Amesema Mchungaji Gabriel.
Ufunuo mkubwa uiliopo ndani ya kitabu hiki utafungua watu wote bila kuchagua dini sababu imezungumzia madhabahu ya kiroho hivyo watu wanunue na wasome watapata vitu vizuri.
Hayo ameyazungumza Edgar Mwakyusa katika uzinduzi wa kitabu cha Nguvu ya utendaji wa madhabahu ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika katika Kanisa la Bethlehem Bread Home Church lililipo Kigamboni Darajani .
“Nikupongeze kwa kuandika kitabu hiki kwa lugha tatu ambapo umewagusa watu wanaotumia Lugha ya kiswahili, Kingereza na Kifaransa hivyo kitafikia watu wengi zaidi”amesema Mwakyusa.