Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amemwakilisha Waziri wa TAMISEMI kuzindua mafunzo kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa Novemba 27 mwaka huu na kuwataka kufanya kazi yao kwa uadilifu ili kuhakikisha wanakuwa kiungo bora kati ya Serikali na wananchi kwa kuwatumikia ipasavyo wananchi na kukomesha migogoro ya ardhi katika maeneo yao
Akizungumza leo Disemba 16, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi wa serikali za mitaa kushirikiana na viongozi wa Dini kuendelea kuhamasisha amani ya Nchi na kusimamia vyema R nne za Rais Dkt Samia ili kuwa na jamii bora
RC Chalamila amewataka viongozi wa serikali za Mitaa kutambua kuwa madaraka waliyonayo ni ya wananchi waliowachagua hivyo wanapaswa kuwatumikia vizuri kwa kutatua changamoto zao hususani huduma muhimu za kijamii sanjari na ulinzi na usalama kwenye mitaa
Aidha amewataka kushirikiana vyema na watendaji wa Mitaa na kuwa wabunifu bila kuathiri mnyororo wa fedha za serikali huku akisisitiza kuepuka kuwaingiza wananchi kwenye migogoro ya ardhi
Kwa upande wake Katibu tawala wq mkoa wa Dar es salaam Dkt Toba Nguvila amesema mafunzo hayo yatakua ya siku mbili kwa wenyeviti wa wilaya zote pia yatafanyika kwenye kila Wilaya ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchu kwa ufanisi mkubwa.
Mwisho RC Chalamila ameagiza taasisi mbalimbali zilizoko katika Mkoa huo kuandaa mafunzo kwa wenyeviti wa Mitaa ili kuwawezesha kuwa na uelewa wa majukumu ya taasisi hizo na iwe rahisi kutoa ushirikiano ” Taasisi ya kwanza ambayo nimeshaielekeza TRA na taasisi zingine zifuate kama DAWASA na TANROAD