36 views 5 mins 0 comments

MCHENGERWA:ATANGAZA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025

In KITAIFA
December 16, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA



Zoezi la Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka, 2025 kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji limekamilika na wanafunzi wote wenye sifa ya kujiunga Kidato cha Kwanza wamepata nafasi ya kujiunga na Kidato cha Kwanza bila ya kuwepo kwa chaguo la Pili kama ilivyokuwa awali.

Hii imetokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika Sekta ya Elimu kwa kuhakikisha kila Mtoto wa Kitanzania anapata fursa ya kupata elimu.


Hayo Ameyasema Leo Tarehe 16 Disemba 2024 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesema jumla ya Wanafunzi 974,332 waliohitimu Elimu ya msingi mwaka 2024 tayari wamepangiwa Shule za sekondari ambao wataanza Januari 2025.

Amesema kuwa chaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka, 2025 umezingatia kigezo cha ufaulu wa mtahiniwa anayechaguliwa. Kila mtahiniwa aliyefanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka, 2024 na kupata jumla ya alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300 amechaguliwa na kupangiwa Shule ya Sekondari ya Serikali.

“wanafunzi 974,332 sawa na asilimia 100 ya wanafunzi wote waliokuwa na sifa ya kuchaguliwa wakiwemo Wasichana 525,225 na Wavulana 449,107. Wanafunzi hao ni wale waliofanya na kufaulu Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka, 2024”.Amesema Mchengerwa

SERIKALI KUGAWA SHULE ZA SERIKALI KATIKA MAKUNDI MATATU

Serikali imetambua Kwa kila mwanafuzi ambae alie weza kufaulu kupangiwa shule za sekondari Katika makundi matatu Ambapo ni za kutwa na za bweni

Shule za Sekondari za Bweni za Wanafunzi wenye ufaulu wa Juu (Special Schools), Shule za  Amali za Kihandisi (Ufundi) na Bweni Taifa. Shule za Bweni ni za Kitaifa hivyo, zimepangiwa Wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuzingatia mgawanyo wa nafasi uliobainishwa na vigezo vilivyowekwa ili kuimarisha Utaifa.

Mchengerwa amebainisha kuwa Nafasi katika Shule za Wanafunzi wenye Ufaulu wa Juu zimegawanywa kwa kila Mkoa kulingana na idadi ya watahiniwa wa Darasa la Saba waliotahiniwa katika Mkoa husika kwa kutumia Kanuni ya kugawa nafasi hizo Kitaifa.

“Nafasi zilizotolewa kwa Mkoa zimegawanywa sawa kwa Halmashauri zote bila kujali idadi ya watahiniwa waliotahiniwa katika Halmashauri. Shule hizi ni Msalato, Mzumbe, Kilakala, Kibaha, Ilboru, Tabora Girls na Tabora Boys”.

“Shule za Sekondari za Bweni za Amali za Kihandisi ni Tanga Tech, Moshi Tech, Musoma Tech, Bwiru Boys, Ifunda Tech, Iyunga Tech, Mtwara Tech, Mwadui Tech na Chato Tech”.

Halikadhalika jumla ya Wanafunzi 974,332 wakiwemo wasichana 525,225 na wavulana 449,107 ikijumuisha Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum 3,067 (wasichana 1,402 na wavulana 1,665) wamechaguliwa na kupangwa katika Shule za Sekondari za Serikali kwa ajili ya kuanza masomo ya Kidato cha Kwanza mwaka, 2025 kwa mgawanyo

(a) Shule za Wanafunzi Wenye Ufaulu wa Alama za Juu:
Jumla ya Wanafunzi 809 wakiwemo wasichana 329 na wavulana 480 wamechaguliwa kujiunga katika Shule za Sekondari ambazo hupokea Wanafunzi wenye ufaulu wa Alama za Juu. Shule hizo ni Ilboru, Msalato, Kibaha, Kilakala, Mzumbe, Tabora Boys na Tabora Girls. 

(b) Wanafunzi Waliochaguliwa Shule za Amali za Kihandisi:
Jumla ya Wanafunzi 1,174 wakiwemo wasichana 197 na wavulana 977 wamechaguliwa kujiunga na Shule za Amali za Kihandisi. Shule hizo ni Ifunda Tech, Bwiru Boys, Mwadui Tech, Iyunga Tech, Moshi Tech, Mtwara Tech, Musoma Tech, Tanga Tech na Chato Tech.

Shule za Bweni Taifa:
Jumla ya Wanafunzi 6,810 wakiwemo wasichana 5,199 na wavulana 1,611 wamechaguliwa kujiunga na Shule za Bweni Taifa. Kati ya wanafunzi hao, Wanafunzi Wasichana 3,320 wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Wasichana za Sayansi za Mikoa katika mikoa yote.

Shule za Kutwa
Jumla ya Wanafunzi 965,539 wakiwemo wasichana 519,500 na wavulana 446,039 wamechaguliwa kujiunga katika Shule za Sekondari za Kutwa ambazo hupokea wanafunzi kutoka katika eneo la karibu na shule ya Msingi aliyosoma Mwanafunzi husika.

Mchengerwa amebainisha kuwa Serikali ilifanya maandalizi mapema ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote watakaofaulu Mtihani wa kumaliza Darasa la Saba mwaka, 2024 wanajiunga na Elimu ya Sekondari ifikapo Januari, 2025. Kutokana na maandalizi hayo Wanafunzi wote 974,332 wakiwemo wasichana 525,225 na wavulana 449,107 waliofaulu Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi 2024 wataanza muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2025 utakaoanza tarehe 13 Januari 2025.

/ Published posts: 1588

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram