14 views 11 secs 0 comments

POLISI WAKAMATA WEZI WA SHEHENA ZA NYAYA ZA SHABA ZILIZOIBIWA ZA TRC NA TANESCO

In KITAIFA
December 15, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Polisi Mkoa wa Kipolisi Rujifi inawashikilia Watu wawili, mmoja akiwa na asili ya Kiasia kwa tuhuma za kukutwa na shehena ya nyaya za shaba zilizoibwa katika Miundombinu ya Umeme – TANESCO na Shirika la Reli Tanzania (TRC).

taarifa ya Jeshi la polisi imeeleza kuwa Watuhumiwa hao walikutwa na copper block 426 zenye uzito wa kilogramu 7,728 na Cooper Wire zenye uzito wa kilogramu 2628.5 ambazo ni  mali za TANESCO zilizoibwa pamoja na Waya za Copper za TRC zenye uzito wa kilogramu 430.

Nyaya hizo zilikuwa zikisafirishwa katika gari aina ya Fuso kutoka kiwandani kwenda mafichoni kufuatia msako wa jeshi la Polisi unaoendelea Mkoani humo.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rujifi limetoa wito kwa Wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano katika kubaini, kuzuia na kuwakamata wale ambao hawataki kufuata njia halali za kujipatia kipato na badala yake wanahujumu miundombinu ya Serikali.

/ Published posts: 1588

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram