Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Benki ya Equity Tanzania, kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imepanda miti 10,000 katika Shule ya Sekondari ya Kirungu, Kijiji cha Kirungu, Wilaya ya Buhigwe, Mkoa wa Kigoma. Miti iliyopandwa ni aina ya Misindano ya asili (Pines), kwenye eneo la shule lenye ukubwa wa hekta 9, kwa lengo la kuhifadhi uoto wa asili na kupunguza athari za mmomonyoko wa udongo.
Benki ya Equity ina lengo la muda mrefu la kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti kila mwaka. Hii ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Uimarikaji na Urejeaji Uchumi wa Tanzania (ARRP) chini ya nguzo ya Kijamii na Kimazingira, inayolenga kuimarisha uhimili wa mazingira na kuchangia maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi kwa jamii zetu.
Shughuli hii imeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina.