Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Wizara ya maliasili na utalii Tanzania imesema kuwa itaendelea kuumga mkono juhudi za serikali chini ya raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia suluhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na katibu mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii Dkt.Hassan abbas wakati akitangaza kufanyika kwa uzinduzi wa Tuzo ya utalii na uhifadhi itakayofanyika Disemba 20 ,2024 mwaka huu jijini Arusha ambapo Tanzania kuwa mara ya kwanza kutoa Tuzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ambao wanakumbukwa kwa kutoa mchango ulioiwezesha sekta hiyo ya utalii kuwa na mafanikio makubwa
Katika hatua nyingine Dkt.Hassan abbas ameweza kuzungumzia Tuzo ambazo Nchi imezipata dunianรญ na afrika kiujumla amesema kuwa tuzo hizo zimetokana na Taifa kuwa na vivutio Bora na ambavyo vimekuwa vikichangia pato la Taifa Katika nyanja mbalimbali za kiutalii na akatatolea mfano mbuga za wanyama kama Serengeti , Ruaha, Ngorongoro pamoja na kuwepo na makumbusho ya kale ni miongoni mwa vitu vinavyosababisha Taifa kuwa na vivutio katika suala zima la kuingiza watalii nchini