29 views 9 secs 0 comments

RAIS SAMIA ARUDISHA TABASAMU NGORONGORO

In KITAIFA
December 06, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan atoa maagizo mazito baada ya kukutana na kuzungumza na wananchi wa jamii ya Kimasai wa Ngorongoro.

Moja kati ya maagizo hayo ni kuundwa kwa tume ya malalamiko itakayobeba kero na changamoto zinazowakabili wananchi hao baadhi yao waliokuwa wakihama kwa hiari kuelekea Msomera Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga.

Maamuzi hayo ya Rais Dkt. Samia kuzungumza na wananchi hao kimekuwa cha kishujaa na kusifiwa na Wadau wengi wa Haki za kibinadamu ambao wamependezewa na kitendo hicho kilichoacha kicheko kwa wananchi hao baada ya kuketi na Rais Dkt.Samia.

โ€œImetupa faraja sana kukaa na Rais wetu mpendwa na kutoa kero zetu zilizokuwa zikitusumbua kwa muda mrefu lakini sasa tumeona tumepata suluhu na tumeshapoa na vidonda vya muda mrefuโ€ Alisema mmoja Kiongozi wa jamii hiyo ya wamasai.

/ Published posts: 1588

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram