Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
IMEELEZWA kwamba Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kutoa Sh bilioni 429.1 kwa ajili ya uwekezaji katika bandari ya Tanga, sasa matunda yameanza kuonekana.
Rais Samia alitoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya uboreshaji wa bandari hiyo. Akizungumza jijini Tanga, meneja wa bandari hiyo, Masoud ,Mrisha, alisema fedha walizopewa kwa ajili ya uboreshaji katika bandari ya Tanga, umeleta matunda.
Mrisha alisema maboresha makubwa yaliyofanywa katika Bandari hiyo wateja wameongezeka tofauti na ilivyokuwa kabla ya uwekezaji huo. Kwa sasa Bandari inauwezo wa kuingiza mizigo mikubwa hasa baada ya kujenga bandari kavu katika eneo lao la Mwambani.
Meneja huyo alisema kutokana na uwekezaji huo, meli 17 za mizigo zimekuja kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Julai hadi Novemba mwaka huu.
Pia alisema maboresho makubwa yaliyofanywa katika Bandari hiyo meli haziwezi kukaa bandarini zaidi ya saa 72 kwa maana ya Siku tatu bila kuondoka.
Alisema ufanisi wa kazi umeongezeka, kwani huchukua saa 72 kuhudumia meli.
Mrisha alisema kwa sasa meli zinatoka moja kwa moja China na magari makubwa yameongeza ambayo yanapeleka migizo Zambia, Dr Congo na Zimbabwe. Meneja huyo alisema bila Rais Samia wa kuwapatia fedha wasingepata mafanikio hayo.
Alimshukuru Rais kwa kutoa fedha hizo zilizowezesha kufanya maboresho makubwa.
Naye Amri Sufiani ambaye ni mdau wa Bandari huyo, alimshukuru Rais Samia kwa uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo. Sufiani alisema alisema Rais Samia amefanya jambo kubwa baada ya kutoa sh bilioni 429.1 kwa ajili ya kupanua kina cha
Bandari na vifaa.
Alisema kutokana na hilo kusababisha meli nyingi kufika Tanga na tangu Julai hadi Novemba 29, meli 17 zimefika katika bandari huyo.
Pia alisema uwekezaji uliofanywa umekuza uchumi katika sekta hiyo, lakini imefungua fursa mkoa wa Tanga na Tanzania. Mdau huyo alisema vijana wengi wanapata ajira na madereva wanapata tenda yangu kufunguliwa kwa Bandari ya Mwambani.
Kwa upande wake, Brown Silivant ambaye ni wakala wa forodha mwakilishi wa kampuni ya ILS Ltd, aliishukuru serikali kwa maboresho makubwa ya ujenzi wa gati. Silivant alisema kabla ya uwekezaji huo zilikuwa zinafika mbili kwa mwezi, lakini kwa sasa zinafika meli moja hadi mbili baada ya Siku sita hadi 10.
Silivant alisema kazi zimeongezeka na wanawahudumia wateja kwa ufanisi mkubwa. Mwisho