19 views 33 secs 0 comments

‘GENERATION’ SAMIA YAIBUKA NA KISHINDO

In MICHEZO
December 04, 2024



Na mwandishi wetu … Dodoma

Programu mpya ya vijana inayojulikana kama Generation Samia (Gen S) imezinduliwa rasmi, Desemba 2, 2024, jijini Dodoma, kwa lengo la kuwaunganisha vijana wa Kitanzania kutoka sekta mbalimbali na kuwajengea mtandao wa fursa za maendeleo. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, msemaji wa @Gen_samia, Sonata Nduka, amesema programu hiyo inalenga kuwa chachu ya mafanikio kwa vijana, ikiwakutanisha kutoka nyanja tofauti kama ujasiriamali, biashara, michezo, usafirishaji, na ujenzi.

Sonata amesema Gen S inalenga kufanikisha ndoto za vijana kupitia juhudi za pamoja huku ikichagiza matumizi ya mazingira rafiki yaliyowekwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha uchumi wa vijana. 

Katika hatua ya kuimarisha mtandao wa vijana, Gen S imeandaa tukio la mbio za pamoja lijulikanalo kama Gen S Jogging, litakalofanyika Jumamosi, Desemba 7, 2024, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. 

Mbio hizo zitaanza saa 12 asubuhi na kumalizika saa 3 asubuhi, zikiwaleta pamoja vijana kutoka makundi tofauti, ikiwa ni pamoja na vikundi vya jogging, wafanyabiashara, wafanyakazi wa sekta binafsi na serikali, pamoja na wanamichezo. 

Sonata amesema tukio hilo si tu fursa ya kujenga mtandao wa kijamii na kiuchumi bali pia litakuwa sehemu ya burudani kwa vijana wa mjini.

/ Published posts: 1536

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram