Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
DKT. Biteko apongeza Wananchi Kujitokeza kwa wingi*
Awahimiza kujitokeza kuwachagua viongozi*
Watanzania katika maeneo mbalimbali ya nchi wamejitokeza kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wao ngazi ya Serikali za Mitaa.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametimiza haki yake ya Kikatiba katika Kata ya Bulangwa, Wilayani Bukombe, Geita kisha akawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 27, 2024 mara baada ya kupiga kura katika kituo cha kupiga kura cha Shule ya Msingi Bulangwa wilayani Bukombe mkoani Geita.
“ Zoezi la kupiga kura linaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi nawapongeza kwa hilo. Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti kwa sababu ya hamasa kubwa ya kushiriki,” amesema Dkt. Biteko.
Amesisitiza “ Ninaomba watu wote waliojiandikisha watumie haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kwa wingi na kwenda kupiga kura,”
Kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizinduliwa Novemba 20, 2024 na kuhitimishwa Novemba 26, 2024 baada ya wagonbea kujinadi na kuomba kura kwa wananchi.