Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA TANGA
Yaibuka Mshindi wa 3 Mchezo wa Kuvuta Kamba (Me)
Timu ya wavuta kamba (Me) ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) leo Novemba 23, 2024 imeibuka mshindi wa 3 katika mchezo wa Kuvuta Kamba baada ya kuishinda timu shindani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) katika mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) ambayo yanatarajiwa kufikia ukingoni Novemba 24, 2024 Jijini Tanga.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Kapteni wa timu ya Kamba (Me) ya TAWA Jumanne Athumani amesema ushindi walioupata umekuwa ni faraja kubwa si tu Kwa wachezaji hao bali Taasisi Kwa ujumla kwani ni takribani miaka 10 sasa wamekuwa wakipambana kufikia hatua hiyo bila mafanikio.
“Nimepende kumshukuru Mungu kwa ushindi huu tulioupata, tumecheza na jirani zetu kabisa JU 01 Ngorongoro, mchezo ulikuwa mgumu na wa nguvu nyingi sana, mchezo ambao ni wa jasho na damu” amesema Kapteni Jumanne Athumani
“Kwa mara ya Kwanza timu yetu imepambana kuweza kuleta kikombe hiki ambacho tumekitafuta takribani miaka 10 bila kukipata ” ameongeza Jumanne.
Aidha Jumanne ameishuru Menejimenti ya TAWA inayoongozwa na Kamishna wa Uhifadhi Mabula Misungwi Nyanda Kwa kuwaamini na kuwapa fursa ya kushiriki mashindano hayo ambayo wameyatumia vyema kutangaza utalii wa ndani Kwa vivutio vinavyopatikana katika maeneo yaliyo chini ya usimamizi wa taasisi hiyo.
Mashindano haya yaliyoshirikisha Mashirika mbalimbali ya Umma , Makampuni na Taasisi Binafsi yalianza Novemba 10, 2024 na yanatarajia kufikia ukingoni kesho Novemba 24, 2024 ambapo TAWA ilishiriki katika michezo ya mpira wa miguu, Pete, Riadha na Mchezo wa Kuvuta Kamba.