Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amejizolea umaarufu huku akipongezwa na Taasisi ya haki za binadamu Duniani kwa kuwapa faraja wananchi wa Ngorongoro.
“tunapenda kutumia fursa hii kumshukuru na kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua nzuri aliyoichukua ya kutuma wajumbe wake wakati wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro wakiwa katika maandamano yaliyodumu kwa siku tano.
Uamuzi huo wa kutuma watu wa kusikiliza vilio vya wananchi na kuagiza vilioo vyao vifanyiwe kazi vimeonyesha busara na hekima ya Mhe Rais. Kwa muda mrefu watetezi wa haki za binadamu tumekuwa tukishauri uongozi wa juu wa nchi ukutane na wananchi, na mara baada ya Mhe Rais kutuma wajumbe wake tumeanza kuona faida ya hatua hii kwa wananchi wa Tarafa hii.
Pamoja na kwamba serikali ndio imelalamikiwa kusababisha changamoto hizi, kitendo cha Mhe Rais kuamua vikwazo hivi viondelewe imeleta matumaini mapya kwa watu wa Ngorongoro, kimetufurahisha sisi watetezi wa haki za binadamu na pia hatua hii inalinda taswira ya nchi katika eneo la haki za binadamu na utawala bora”.
Baada ya kufanya ziara mwaka 2024 katika Tarafa ya Ngorongoro, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umejionea hali ya haki za binadamu pamoja na huduma za kijamii katika tarafa ya Ngorongoro. Tunatambua na kuthamini juhudi za hivi karibuni zilizofanywa na Serikali kurejesha huduma muhimu za kijamii katika Tarafa ya Ngorongoro, eneo ambalo liliathiriwa kwa kiasi kikubwa na kusitishwa kwa huduma hizi kwa takriban mwaka mzima. Kusitishwa kwa huduma hizo hasa kuanzia mwaka 2022 kuliathiri jamii za asili na wafugaji katika eneo hilo ambalo ni mseto.
Taarfa ya Ngorongoro yenye idadi ya watu 100,000 ina jumla ya kata 11, Vijiji 25, Shule za Msingi 22, Shule za Secondary 3, Hosptali Moja ya Mission na Vituo vya Afya na Zahanati 13.
Vyote hivi vimekuwa na changamoto nyingi za kuwahudumia wananchi kwa miaka minne sasa. Pamoja na kwamba bado ukarabati wa maeneo mengi ya huduma za kijamii haujaanza. Tumejionea mikakati na hatua za awali za urejeshwaji wa huduma za msingi kama elimu, maji n.k