Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Mamlaka ya Mapato Nchini Tanzania( TRA) kwa kushirikiana na Shirika la viwango Zanzibar (SBZ) imesaini hati za makubaliano katika kwenda kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa pamoja.
Hayo yamesemwa Jijini Dar e salaam na Kamishina Mkuu wa mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema kuwa TRA inasimamia shughuli za forodha kutoka bara hadi Zanzibar hivyo inaenda kurahisisha mifumo ambayo inatumia forodha Zanzibar.
Katika makubaliano haya tunaenda kushirikiana kwa kubadilishana Taarifa mbalimbali kwa kutumia mifumo huku mifumo ya ZBS ikiunganishwa na mifumo yetu kabla ya
kuruhusu mizigo itoke kwenye Bandari ya Zanzibar.
Aidha Kamishina Mwenda Aliongeza kuwa kabla ya kuruhusu mizigo kutoka kwenye bandari ya Zanzibar itakaguliwa na iwe imekidhi viwango huku taarifa mbalimbali zikiwemo ili kwenda kukuza na kuendeleza biashara.
“Kupitia makubaliano haya tunaenda kupunguza Changamoto ya mizigo bandarini ambayo ilikuwa inapitia bandari ya zanzibar Pia niwahakikishie wafanyabiashara wa bandari kutoka Zanzibar TRA na ZBS zimekuwa karibu na itaenda kurahisisha ukaguzi wa mizigo inayopita Bandari ya Zanzibar ” Amesema Kamishina Mwenda
Naye Mkurugenzi kutoka Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) Yusuph Nassor Ameongeza kuwa mapato ambayo tunapata ZBS ni kutokana na ushirikiano kutoka TRA hivyo tunapata mchango mkubwa na kuweza kuimarisha mifumo yetu kwa pamoja kupitia utendaji kazi.
Kwa upande wetu Zanzibar tunataka tusitoe huduma kwa mtu yeyote ambaye hajasajiliwa na TIN namba hivyo tunaenda kuhakikisha tunaingiza mizigo kwa upande wa zanzibar kwa mfanyabiashara Mjasiriamali, au mwenye kiwanda anatakiwa kukaguliwa na TRA