Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mvua kwa msimu wa Novemba 2024 hadi Aprili 2025, ikisisitiza umuhimu wa maandalizi katika sekta mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa Leo Kamu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Ladislaus Chang’a alisema mvua za msimu zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya pili na ya tatu ya Novemba mwaka huu na ambazo zitaendelea hadi mwishoni mwa mwezi Mei 2025 katika maeneo mengi ya nchi.
Hata hivyo, baadhi ya mikoa kama Kigoma, Tabora, na Katavi inatarajiwa kuanza mvua za msimu mapema zaidi.
‘Mvua za Vuli zilizoanzq Oktoba hii Hadi Desemba 2024 zinatarajiwa kuwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko usioridhisha katika maeneo kadhaa. Hali hii inahusishwa na joto la bahari linaloonekana kuwa wastani hadi juu kidogo katika maeneo ya Bahari ya Hindi na Atlantiki,” alisema Kaimu Chang’a.
TMA imebainisha athari mbalimbali zinazoweza kutokea kutokana na mwenendo huu wa hali ya hewa, ikiwemo changamoto katika kilimo, mifugo, utalii, usafiri, na afya ya umma.
“Kwa mfano, athari katika kilimo ni pamoja na mafuriko na upungufu wa unyevunyevu unaoweza kuathiri ukuaji wa mazao. Wafugaji wanashauriwa kujiandaa kwa upungufu wa malisho na maji, huku sekta ya afya ikihimizwa kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana na magonjwa yanayoweza kuzuka kutokana na maji kutuama na mazingira ya unyevunyevu, ” alisema.
Alisema kuwa ili kuongeza tija na ufanisi mamlaka imeandaa utabiri maalum kwa ngazi ya wilaya katika mikoa inayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka huduma ambazo tabiri zake zinatarajiwa kusaidia wadau katika sekta mbalimbali kuchukua hatua madhubuti za kupunguza athari zinazoweza kujitokeza na kuimarisha ustawi wa kijamii na kiuchumi.