33 views 5 mins 0 comments

MIRADI YA DMDP II YAIVA DAR

In KITAIFA
October 28, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA



Mikataba yasainiwa rasmi yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.18

Waziri Mchengerwa amshukuru Rais Dkt Samia kwa kuweka historia ya miradi mikubwa


DAR ES SALAAM

HISTORIA imeandikwa katika Jiji la Dar es Salaam, baada ya  utiaji saini mikataba nane ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Halmashauri tano za mkoa huo, kupitia Mradi wa Uendelezaji Jiji (DMDP II) awamu ya pili, wenye  thamani ya zaidi ya Shilingi trioni 1.18.

Halmashauri zitakazo nufaika ni Tekeme, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na Ubungo huku mradi huo ukiwa na jumla ya kilometa mraba za lami  250, mifereji yenye kilometa 90, stendi za mabasi tisa, masoko 18 na madambo matatu ya taka ngumu.

Akishuhudia utiaji saini jana katika hafla ya mradi huo, iliyofanyika Wilaya ya Temeke, viwanja vya Mwembe Yanga, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, alimshukuru Rais Dkt.Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kufanikisha mradi ulioweka historia kubwa na kubadilisha jiji hilo.

Aliwaagiza viongozi wa Mkoa huo, Wizara na TANROADS kusimamia vyema mkadarasi kutekeleza kazi kwa weledi na kukamilisna kwa wakati Kwa hawataongeza muda.

Pia, alimuagiza Katibu Mkuu kuhakikisha acheleweshi  suala la  kuanzisha Jiji  la Dar es Salaam lifanyike kabla ya 2025, ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia kuinua uchumi wa wananchi ambapo walisema wanaendelea na mradi wa bonde la  mto msimbazi lenye hekta 57, ambapo mchakato wake unaendelea.

“Jambo hili linaonesha nia nje ya serikali ya Rais Dk.Samia  katika utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo unatarajiwa kuboresha miundombinu mbalimbali barabara, masoko, vituo vya mabasi, miradi ya taka ngumu.

“Nawaagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI na Mtendaji Mkuu wa TANROADS kuhakikisha wanasimamia vizuri utekelezaji wa miradi hiyo ikamilike kwa wakati na ubora, kwani hawataongeza muda kwa mkandarasi asipokamilisha kwa wakati,” alisisitiza.

Waziri Mchengerwa aliwataka kuhakikisha wanazingatia uhitaji wa wananchi,  katika utekelezaji wa mradi hiyo, isijengwe maeneo ambayo sio rafiki na wananchi, masoko zaidi ya 20 yatakayojengwa kuhakikisha yanajengwa penye uhitaji huku akizitaka halmashauri kuhakikisha wanawajengea uwezo wafanya biashara.

Alisema hakuwezi kuwa na Jiji zuri kama miundombinu ya barabara halijaboreshwa, ambapo fikra za ujenzi wake ulifanywa na Rais Dk.Samia kwa lengo la kusogeza huduma hizo  karibu na jamii.

Alieleza, ujenzi wa barabara utaondoa foleni, kusogeza uchumi karibu na wananchi, kupunguza gharama za maisha na kukua kwa uchumi wa wananchi ikiwa ni maoni ya Rais Dkt. Samia kuinua uchumi wa wananchi.

Alisema mradi huo ni ndoto za Watanzania, ambapo yalikuwa maono ya Rais wa kwanza Mwalimu Julius Nyerere ambapo Rais Dkt.Samia ameendelea kuyaishi ikiwa ni zaidi ya Kilometa 250.

“Kwa ujenzi huuu ni meona hakuna sababu kuwa kwanini hatuna Jiji la Dar es Salaam, watu wengi watakuja Dar es Salaam na kuchochea ukuaji wa kiuchumi, hivyo mchakato wa Jiji uharakishwe,” alisema

Alimuagiza Katibu Mkuu, kuzungumza na wataalamu waaharakishe suala la uboreshaji wa mradi wa mto msimbazi kutekelezwa haraka kwa kupata wazabini utekelezaji uanze.

Kuhusu gharama  za mradi huo, alisema utagharimu dola za Kimarekani, 438 zaidi ya Shilingi trioni 1.182 ambapo ni za mikopo na fedha za ruku kutoka Uholanzi huku akiwashukuru wabia wote ikiwemo Benki ya Dunia na serikali y Uholanzi ambao wamedhaniria kukomboa wananchi kiuchumi.

“Leo tunashuhudia utoaji Saini wa miradi nane yenye urefu wa kilometa 168 .12 za barabara jijini Dar es Salaam, ambapo zabuni 19 zimeshatangazwa na zabuni 8 zimetiwa saini leo zenye thamani ya sh. bilioni 190  kujenga kilometa 63,” alisema.

Alisema mikataba itakayobaki  ni Ile yenye thamani ya sh. bilioni 262 zitakazo jenga barabara kilometa 104.

Aliagiza TARURA, kuhakikisha wanaharakisha upatikani wa wazabini kwa kuzingatia wakandarasi wazawa wenye ubora.

Aliwapongeza wabunge na viongozi mbalimbali wa halmashauri zote kwa kazi kubwa wanayoifanya, hivyo wahakikishe wanawasimamia vyema wakandarasi hao wasicheleweshe utekelezaji wa miradi hiyo.

“Tunakukabidhi Mkuu wa Mkoa, miradi hii, mimi nitakudai wewe kawasimamia vizuri wakandarasi, leo tunawakabidhi, kesho kaeni nao, wawaambie lini wataikamilisha wasicheleweshe,” alisema.

Aliwapongeza wabunge wa CCM kwa kuhakikisha wanapigania miradi hiii kwa nguvu kubwa, huku akiwataka viongozi hao kwenda sambamba na wakandarasi hao kuhakikisha wanafanya kazi kusudiwa.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram