Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Wakuu wa Polisi Afrika Mashariki Wakutana Dar es Salaam Kupanga Mikakati ya Kukabiliana na Uhalifu wa Kikanda
Wakuu wa Polisi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana jijini Dar es Salaam Oktoba 25 ,2024 kwa mkutano wa 8, wakilenga kujadili changamoto za amani na usalama katika ukanda huo. Akizungumza kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai CP Ramadhani Kingai amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kupambana na uhalifu unaovuka mipaka, ugaidi, usafirishaji wa binadamu, na madawa ya kulevya.
Kingai ameeleza kuwa ni muhimu kwa nchi wanachama kuimarisha miundombinu ya usalama na kubadilishana taarifa za kijasusi ili kukabiliana na vitisho vya uhalifu wa kisasa. Aidha, amehimiza washiriki wa mkutano huo kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania. Mkutano huo unatarajiwa kuleta mikakati madhubuti inayolenga kuifanya Afrika Mashariki kuwa salama kwa biashara na maendeleo.