Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 24, 2024 ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya awali ya ujenzi wa zaidi ya kilomita 168 za barabara za Mkoa wa Dar es Salaam, zitakazojengwa na mradi wa DMDP awamu ya pili.
Akizungumza katika hafla hiyo mkoani Dar es Salaam, Mchengerwa amesema jumla ya zabuni 19 tayari zimetangazwa na zipo katika hatua mbalimbali za manunuzi ambapo kati ya zabuni hizo leo umefanyika utiaji saini wa mikataba nane ya awali yenye thamani ya shilingi Bilioni 190.04 inayokwemda kujenga jumla ya kilomita 63.66 za barabara.
Mchengerwa amesema kwa mikataba iliyobaki yenye thamani ya shilingi Bilioni 262.46, zitajengwa kilomita 104.56 za barabara ambapo ndani ya mwezi Novemba 2024 itakuwa imekwishasainiwa.
Mradi wa DMDP awamu ya pili unatarajiwa kuboresha miundombinu mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam zikiwemo barabara, masoko, vituo vya mabasi, mifereji ya maji ya mvua, maeneo ya wazi pamoja na usimamizi wa taka ngumu.
Mchengerwa amesema jumla ya zabuni 19 tayari zimetangazwa na zipo katika hatua mbalimbali za manunuzi ambapo kati ya zabuni hizo leo umefanyika utiaji saini wa mikataba nane ya awali yenye thamani ya shilingi Bilioni 190.04 inayokwemda kujenga jumla ya kilomita 63.66 za barabara.
Mchengerwa amesema kwa mikataba iliyobaki yenye thamani ya shilingi Bilioni 262.46, zitajengwa kilomita 104.56 za barabara ambapo ndani ya mwezi Novemba 2024 itakuwa imekwishasainiwa.
Mradi wa DMDP awamu ya pili unatarajiwa kuboresha miundombinu mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam zikiwemo barabara, masoko, vituo vya mabasi, mifereji ya maji ya mvua, maeneo ya wazi pamoja na usimamizi wa taka ngumu.
Amesema Mkoa wa Dar es salaam unatakiwa kuwa Kioo cha nchi na wageni wote wanapokuja hapa wanatakiwa kuona sura ya Tanzania hivyo inapaswa kuwa na chombo kinachoratibu maendeleo yake na kuhakikisha kuwa mipango yote ya maendeleo inayofanyika na inakua na muunganiko.
Ameongeza kuwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji ma Dar es salaa awamu ya Pili (DMDP II) kuna miradi mikubwa inayotekelezwa kama ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara na uendelezaji wa bonde la mto msimbazi hivyo miradi mikubwa kama hiyo kwenye halmashauri inahitaji chombo cha kusimamia.
“Hata majiji makubwa duniani yote yanakuwa na ‘Metropolitan City’ na sio halmashauri zinazojitemea kila moja inapangwa kivyake kunatakiwa kuwa na chombo ambacho kinaunganisha jitihada zinazofanywa kwenye halmashauri zote na kuzitaribu ili Jiji husika liweze kukua kwa viwango vya kimataifa.”
“Nataka hii Dar es salaam iwe ya viwango na ubora na ukuaji wake uratibiwe kwa taratibu maalumu na sio kukua kiholela tu hii itafanya hadhi ya Dar es salaam isikue haraka na kuwa na hadhi ya kimataifa,”amesema.
Mchengerwa amewataka pia kuzingatia mahitaji ya wananchi hasa kuhakikisha miundombinu inayojengwa ni kweli wananchi wa eneo husika wanaihitaji ili kusiwe na miundombinu inayojengwa halafu haitumiki.
Ameziagiza halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam na halmashauri zote nchini kuhakikisha wakati wa kutekeleza miradi ziwe zimetenga eneo la kuwapeleka wafanyabiashara kwenye eneo la muda kupisha ujenzi, badala ya kuwaondoa bila sehemu mbadala na hivyo kuwachonganisha na Serikali yao.