55 views 2 mins 0 comments

WWF WATOA RIPOTI NZITO,HOFU YA WANYAMA PORI KUPUNGUA YATAJWA

In KITAIFA
October 16, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM




IMEBAINIKA  kuwa idadi ya wanyamapori Duniani imepungua kwa asilimia 73 katika kipindi cha miaka 50 iliyopita Afrika, kwa .upande wake, imeshuhudia upungufu wa asilimia 76, huku sababu kuu zikiwa ni uharibifu wa makazi, uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na viwanda, mabadiliko ya matumizi ya ardhi, ukataji miti uliokithiri, uchafuzi wa mazingira, na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamebainika katika uzinduzi wa ripoti mpya inayojulikana kama  Living Planet Report 2024 iliyotolewa na WWF inatoa tahadhari ya hatari inayokaribia ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa ili kuzuia mifumo ya ikolojia kuvunjika. Uharibifu huu unaweza kusababisha athari kubwa kwa usalama wa chakula, upatikanaji wa maji safi, na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Dk. Amani Ngusaru, Mkurugenzi wa WWF Tanzania, ameangazia hitaji la haraka la kuchukua hatua, akisema: “Ripoti ya LPR 2024 inatoa ishara za mapema kuwa tunakaribia kufikia viwango vya hatari ambavyo haviwezi kurekebishwa. Ni lazima tuchukue hatua kali sasa.”

Dkt Ngusaru amesema kuwa hali hii inaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa maisha ya wanyama kama vile tembo na kifaru, lakini pia kuathiri vibaya watu wanaotegemea mifumo ya ikolojia.
Katika kutoa mwelekeo wa nini Tanzania inapaswa kufanya,
   
     
Mkutano huo, ambao uliwakutanisha wataalamu wa uhifadhi na wadau mbalimbali, ulitilia mkazo umuhimu wa kuchukua hatua sasa ili kuzuia madhara makubwa zaidi kwa mazingira na maisha ya watu.

Dk. Lawrence Mbwambo, Mkurugenzi wa Uhifadhi wa WWF Tanzania, amesema kuwa licha ya ongezeko la wanyama kama vile tembo na kifaru (263) katika miaka ya hivi karibuni, bado kuna kazi kubwa ya kufanywa ili kurudisha hali ya wanyamapori na misitu katika hali ya usalama.

“Hatujafikia kiwango cha kutosha cha kusema kuwa wanyamapori wetu wako salama,” amesema Dk. Mbwambo.

Hata hivyo, Amongeza kuwa juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisha Tanzania inatimiza malengo yake ya uhifadhi wa mazingira ifikapo mwaka 2030.


WWF imetoa wito kwa serikali nchini kuchukua hatua za dharura kuzuia uharibifu zaidi wa mazingira na kuhakikisha mipango ya uhifadhi inatekelezwa kikamilifu.

/ Published posts: 1501

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram