54 views 40 secs 0 comments

SERIKALI IMEANZA KUWEKA MIKAKATI MBALIMBALI YA UTOAJI WA ELIMU KWA WANANCHI KWA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

In KITAIFA
October 16, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko amesema  ifikapo Disemba mwaka 2024, Serikali inatarajia kutoa mitungi  Gesi zaidi ya Laki Nne ambayo itakayowezesha kuwanufaisha Watanzania kwa ajili ya matumizi ya Nishati Safi ya Kufikia.

Biteko ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizindua Soko la nishati Afrika na kufanyika Jijini Dar es Salaam.

Aidh ameeleza kwamba gesi hiyo itagawiwa kwa wananchi kwa gharama nafuu tofauti na bei wanazonunulia Mitaani.

Pia amesema Serikali imeanza kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo utoaji wa Elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Katika hatua nyingine, Doto Biteko ameema ifikapo mwaka 2030 karibu watu Milioni 300 kutoka Nchi za Afrika watakuwa wamefikiwa na huduma ya nishati ya umeme.

Aidha amesema hatua  hiyo imekuja kutokana na Nchi ya Tanzania kuendelea kupiga hatua kwa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini -REA.

Amesema vijiji vipatavyo elfu 12 na vitongoji vyake vitaweza kunifaika na huduma ya umeme.

Amesema kupitia Banki ya Maendeleo ya Afrika imeichagua Tanzania kuandaa Mkutano wa Siku mbili wa masuala ya Soko la Nishati Afrika,  kutokana Nchi kupiga hatua kuwa kwa upande wa Kisera, Usimamizi na usambazaji wa umeme vijini.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram