Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Onesho la Swahili International Tourism Expo (S!TE) mwaka 2024 limehitimishwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa kwa kuingiza takribani wanununuzi 120 wa Kimataifa wa bidhaa za utalii.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Oktoba 13,2024 wakati akifunga Onesho hilo katika ukumbi wa Mlimani City,Dar es Salaam, Waziri wa Maliasi na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana amesema mwitikio mkubwa uliosababisha Onesho hilo kuwa na idadi kubwa ya washiriki ni pamoja na filamu ya The Royal Toure aliyofanywa na Rais Dkt Samia.
โUtalii imekuwa ikichangia Kwa kiasi kikubwa Pato la Taifa kuanzia mtalii anashuka airport,tax anayochukua na hoteli anayofikia pamoja na kule anakotembelea ambapo kote anaacha fedha za kigeni ambazo huchangia Pato letuโamesema
Aidha amesema Ulinzi wa rasilimali za Tanzania ikiwemo Misitu na mbuga ni muhimu sana Kwa Taifa na kipaumbele kwa kila mtu ili kuendelea kustawisha uchumi wa nchi hivyo watanzania wanapaswa kuzitunza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania,Balozi Dr Ramadhan Dau amesema mafanikio waliyopata Kwa mwaka huu ni ishara tosha ya mafanikio ya maandalizi ya Onesho lijalo ambapo Kwa mwaka huu limefanyika Kwa mara ya nane tangu lilipoanzishwa mnamo mwaka 2014.
Naye Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Misitu (TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema Utalii wao kwa kiasi kikubwa upo kwenye Mazingira Ikolojia ambayo ni ya kuona na kuushughulisha mwili na akili hususani kwenye masuala ya kutembea kwenye Misitu, kupumzika, kupanda milima na michezo mbalimbali .
Aidha amesema kuwa fursa hizo zikitumika vizuri zitawafanya watalii kukaa kwa mda mrefu zaidi Tanzania hivyo kuongeza Pato la taifa na uchumi wa watanzania.
Hata hivyo amewahimiza watanzania kushiriki katika kuhifadhi Maliasili za Tanzania ikiwemo Misitu ambayo unatunza mazingira na kuleta hewa Safi.