44 views 53 secs 0 comments

UWT IPO NA RAIS SAMIA UHAMASISHAJI MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA-CHATANDA

In Uncategorized
October 12, 2024

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

Nia ni watanzania wengi zaidi watumie nishati safi ya kupikia*

Asema UWT itaendelea kuishauri Serikali uwepo ya mitungi ya gesi ya gharama nafuu zaidi*

Wanawake na watoto watajwa kuwa waathirika wakubwa matumizi ya nishati isiyo safi*

Mwenyekitiwa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UWT), Mary Chatanda amesema
Jumuiya hiyo itaendelea  kuunga mkono juhudi za Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia  kupitia mkakati uliopo wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Chatanda ameyasema hayo jijini Dodoma  wakati akihamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi na kuanza kupika kisasa kupitia nishati safi ya kupikia.

“Nishati safi ya kupikia upatikanaji wake hivi sasa umekuwa rahisi, pamoja na kuiunga mkono Serikali kwenye ajenda hii, tutaendelea kuishauri  kupunguza zaidi gharama za mitungi ya gesi ili wananchi wengi waweze kuimudu.” Amesema Chatanda

Ameeleza kuwa, utafutaji wa nishati isiyo safi ya kupikia umekuwa hatarishi  kwa wanawake kipindi wanapokuwa maporini wakitafuta kuni kwani wa nakutana na ukatili wa kijinsia na hata katika nyakati wanapochelewa kurejea majumbani.

Amesema nishati safi ya kupikia itawakomboa wanawake na watoto na athari mbalimbali ikiwemo  za kiafya na ukatili waliokuwa wakikutana nao wakati wa utafutaji wa kuni.

Tanzania imeanza kutekeleza Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao  unaelekeza asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.

/ Published posts: 1454

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram