58 views 4 mins 0 comments

UANDIKISHAJI WAPIGA KURA S/MITAA WASHIKA KASI

In KITAIFA
October 12, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA



-DAR/MIKOANI

WAKATI zoezi la uandikishaji wapiga kura likianza kwa siku ya jana nchini hali ya mwitiko wa wananchi imekuwa nzuri huku katika baadhi ya maeneo machache wananchi wajitokeza kwa suasua.

Hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaoatarajiwa kufanyika Novemba 27,  mwaka huu.

Jana katika baadhi ya maeneo Jijini Dar es Salaam gazeti la WAMACHINGA lilishuhudia misururu ya watu kwenye foleni wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kujiandikisha.

Katika eneo la Manzese mwandishi wetu alishuhudia makundi ya watu wakiwa wenye vituo wakijiandisha huku utulivu ukiwa umetamalaki licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu.

RAIS SAMIA

Jana kiongozi wan chi Rais Samia Suluhu Hassan jana aliongoza Watanzania na kujitokeza kujiandikisha katika Daftari ya wapiga kura katika eneo lake alaloshi la kwenye kitongoji chake cha Sokoine kilichopo Kijiji cha Chamwino Ikulu mkoani Dodoma.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza watanzania katika zoezi la kujiandikisha katika daftari hili ili kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024

Ambapo kwa Wilaya ya Ubungo, makundi ya wananchi  wamejitokeza kujiandikisha kwenye vituo 332 vilivyopo kwenye mitaa 90 na kata 14 za wilaya hiyo.

Katika eneo ya Mtaa wa Kilimani ilipotimu saa 5 subuhi Mbunge wa Jimbo la Ubungo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo, alijitokeza na kuandikisha kwenye Daftari la Wakazi wa Mtaa kwa ajili ya kupiga kura.

Akizungumza mara baada ya kujiandikisha Profesa Kitila, alisema kuwa ni wajibu kwa kila Mtanzania kutumia haki yake ya kikatiba kuchagua vongozi anaowataka siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

“Kwanza niwaomba wananchi wa Jimbo la Ubungo na wilaya nzima kwa ujumla kujitokeza kwa wingi wajiandikishe ili waweze kupata haki ya kuchagua viongozi wanaowataka. Msingi wa uongozi huanza na ngazi ya chini ya msingi ambayo ni mtaa, kijiji na kitongoji.

“Na wote tunajua kwamba kwamba uchaguzi wa Mtaa ni muhimu sana kwani viongozi hawa ndio wtoa huduma wa kwanza kwa jamii. Hivyo nichukue nafasi hii kuwaomba sana wananchi wa kata zote nane za Jimbo la Ubungo wajitokeze kwa wingi,” alisema Profesa Kitila

DKT. BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika vituo vya kujiandikisha wapiga kura ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.



Dkt. Biteko amesema hayo jana mara baada ya kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura katika Kituo cha Kujiandikisha Mpiga Kura cha Shule ya Msingi Bulangwa kilichopo Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.

“ Ninawashukuru sana kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ni jambo la muda mfupi ni imaani yangu kuwa mtamaliza kwa wakati ili muweze kwenda kuendelea na shughuli zenu,” alisema na kuongeza  Dkt. Biteko

“ Zoezi hili linaanza leo (jana)  hadi Oktoba 20, 2024. Wananchi wa Bulangwa mjitokeze waandikishaji wamejiandaa vizuri na tunataka tuone orodha ya watu wote ili muda ukifika muweze kupiga kura,” alisema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella alimpongeza Dkt. Biteko kwa kushiriki zoezi hilo la kujiandikisha na kusema kuwa ameonesha mfano kwa wananchi wa Bukombe na kuwataka wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ili washiriki katika uchaguzi wa kidemokrasia.

“ Tuendelee kuwasihi wananchi kutoka kila kitongoji kujiandikisha katika Daftari la Mpiga Kura kwa kuwa yametengwa maeneo ya kutosha ili kuwawezesha wananchi wote wenye sifa muweze kupata fursa hiyo,” alisema Shigella.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Lutengano Mwalyibwa alisema kuwa maandalizi ya kibajeti na miundombinu kwa ajili ya wananchi kujiandikisha yamefanyika na kuwa Jimbo la Bukombe lina vituo 348 na mategemeo ni kuandikisha wananchi 109,124.

/ Published posts: 1454

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram