60 views 2 mins 0 comments

RAIS SAMIA AIWEZESHA REA RUZUKU MITUNGI YA GESI

In KITAIFA
October 09, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

REA kusambaza mitungi ya gesi 3,225 Gairo, yaendelea kugawa majiko banifu kwa wananchi

Na MWANDISHI WETU

-GAIRO

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ruzuku ya bei kwenye mitungi ya gesi inayotolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili Watanzania watumie nishati safi na salama kwa afya zao pamoja na kuhifadhi mazingira nchini.

Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Teknolojia Mbadala na Nishati Jadidifu, Mha. Advera Mwijage wakati akimuelezea Mkuu wa Wilaya ya Gairo na wananchi mara baada ya kutembelea banda la REA kwenye Maonesho ya Samia KILIMO Biashara Expo 2024 yanayofanyika katika Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

“Mhe. Rais Samia ametoa ruzuku ya bei kwenye mitungi ya gesi ili iuzwe kwa bei rafiki, kusambazwa kwa wingi na kila Mtanzania aimudu na atumie nishati hii muhimu,” alisema Mhandisi Mwijage.



Aidha, REA itaendelea kusambaza kwa wingi majiko ya gesi nchini na wilaya ya Gairo pekee jumla ya majiko 3,225 ya gesi yatatolewa kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuitangaza na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Pamoja na hali hiyo aliongeza kuwa REA wameanza kutoa majiko banifu 790 kwa wananchi wa Gairo ambayo ni majiko rafiki, imara REAukwa muda mrefu, yanatunza mazingira na yanatumia kiasi kidogo cha mkaa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Gairo,  Jabir Makame alimshukuru Rais Samia kwa kutoa ruzuku ya bei kwenye mitungi hiyo kwa wananchi wake ambapo itarahisisha upatikanaji wake kwa wingi.

“Wananchi wenzangu wa Gairo, majiko haya ni rafiki kwa matumzi, salama kwa afya zenu, ni msaada mkubwa katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira yetu.

“Nawahimiza kuyanunua ili nishati hii iwe na manufaa makubwa kwenye familia zetu badala ya kuendelea kukata miti kupata mkaa na kuni,” alisema DC Makame.

Wananchi wa Gairo na maeneo jirani ya wilaya hiyo wameendelea kufurahia ruzuku ya bei ya majiko ya gesi na majiko banifu na kuipongeza Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo na kuwataka ambao hawajapata majiko hayo kutembelea banda la REA.

/ Published posts: 1454

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram