49 views 53 secs 0 comments

MIAKA 60 YA HIFADHI YA TAIFA RUAHA, WAZIRI PINDI AZINDUA UTALII WA BALOON

In KITAIFA
October 07, 2024



Waziri Chana azindua Utalii  wa Puto.

Maboresho makubwa ya Miundombinu ya Utalii yaja


Na Happiness Shayo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi,Dkt. Pindi Chana (Mb) amezindua rasmi utalii wa puto  ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.

Uzinduzi huo umefanyika leo Oktoba 7,2024 katika eneo la Korongo View ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.

Akizungumza katika mahojiano maalum ya Kipindi cha Jambo Tanzania ya Shirika la Utangazaji la TBC,  Mhe. Chana amesema mafanikio hayo ni kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  za kutangaza vivutio vya utalii.

“Tunamshukuru Rais Samia kwa kuionesha dunia  vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo mpaka sasa watalii wameongezeka na kufikia milioni 1.8 na mapato ya Taifa  tunachangia asilimia 17% na  fedha za kigeni takribani dola za kimarekani  Bilioni 3.6.

Kuhusu maboresho ya
Miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Ruaha  Mhe. Chana amefafanua kuwa mpaka sasa kuna barabara ya Iringa- Msembe  yenye urefu wa kilomita 104 ambayo inaenda kujengwa.

Aidha, amesema katika Hifadhi ya Taifa Ruaha kutakuwa na uwanja wa ndege sambamba na kutumia uwanja wa ndege wa Nduli uliopo Mkoa wa Iringa ambao  unaendelea kukarabatiwa.

Amesema ndani ya miaka 3  kumekuwa na mabadiliko makubwa ya sekta ya utalii na Serikali inazidi kuboresha maeneo mengi ya Utalii huku akihamasisha wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika hifadhi hiyo.

/ Published posts: 1444

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram