Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Mkurugenzi Mkuu aweka wazi sasa michango yake yafikia trilioni 8.5/-
Achambua namna Serikali ya Awamu ya Sita ilivyotanua wigo wa waajiri na waajiriwa nchini kwa asilimia 70 hadi sasa
-DAR ES SALAAM
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeongezeka kutoka S tirioni 8.4 mwaka 2021 hadi kufikia tirioni 8.5 mwaka 2024 ongezeko hilo likichangiwa kutokana na wingi wa waajiri na waajiriwa.
Hayo aliyasemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii (NSSF)Masha Mshomba kwenye mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Mshomba alisema maboresho ya mfumo wa tehema pia imechangia kuongezeka kwa fedha hizo kwenye mfuko wa hifadhi wa jamii ambapo mpaka kufikia mwaka 2025 wanatarajia kufika asilimia 82 kwenye Tehama ya mfuko huo.
Aidha Mshomba alisema kuwa maboresho hayo ya mfumo wa Tehama yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa usumbufu wa wateja kwenda ofisini kwani wanaweza kufanya kidijitali ambapo inaendana na kasi ya mabadiliko ya Dunia kwenye Tehama.
โSerikali inatoa mchango mkubwa kwenye mfuko huo wa hifadhi ya jamii na wao kama mfuko wanaweka mazingira mazuri ya watumishi, uadilifu pamoja na Tehama.
โNa haya yanatokana na kazi kubwa ambao imefanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye wakati wote amekuwa dira ya maendeleo katika Sekta ya Hifadhi nchini.
โJambo kubwa tunawaomba wanachama wetu kuhakikisha kwamba na kuona kuwa NSSF ni kimbilio lao hasa kwa wale wa sekta rasmi ya ajira na ile isiyo rasmi ambapo tunawaomba wanachama wetu waendelee kuchangia Mfuko wetu,โ alisema Mshomba
Kutokana na hali hiyo Mkurugenzi huyo wa NSSF alisema kuwa Mfuko huo unafanyakazi kwa karibu na Serikali ya Awamu ya sita ambayo imesaidia kukuza ajira kwa asilimia 70.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uwezeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Omary Mziya amesema wameanzisha skimu ya Taifa ya hifadhi ya jamii sekta isiyo rasmi yaani (National Informal Sector Scheme -NISS) iliyoanzishwa mwaka 2018 yenye lengo la kuongeza wigo kwenye hifadhi ya jamii na makundi yasiyonufaika na huduma hizo pamoja na kuchochea maendeleo na kasi ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Naye Meneja wa Mifumo kutoka Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) Mihayo Selemani alisema lengo la matumizi ya tehama kwenye mfuko wa hifadhi hiyo ni kuhakikisha wanachama wote wanapata huduma zote katika lango la huduma kwenye mfuko huo.
Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile aliushukuru uongozo wa NSSF kwa semina hiyo kwa wahariri huku akishauri kuwa mfuko huo uwekezekeze kwenye miradi ya kimkakati pamoja na ajenda ya msingi ya uwekezaji kwa maendeleo ya nchi.