124 views 2 mins 0 comments

WAZIRI MKUU NA MKURUGENZI WA AMREF WATETA

In KITAIFA
October 01, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

MAREKANI

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa alifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Amref Health Africa Dkt. Githinji Gitahi, kando ya Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 79) ambao alishiriki kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan  Jijini New York,

Katika mazungumzo hayo yalifanyika juzi, Majaliwa alilipongeza shirika hilo kwa kazi kubwa inayofanya kwenye sekta ya afya nchini Tanzania na alimuahidi Mkurugenzi Mtendaji huyo kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano ili mipango na malengo ya shirika hilo ya kuisaidia  sekta ya nchini yaendelee kufanikiwa.

Alisema kuwa jitihada ambazo shirika hilo limekuwa likizifanya kwenya sekta ya afya nchini Tanzania zimeendelea kuzaa matunda na kuwezesha kuwafikia watanzania wengi kwenye huduma ya afya

“Kwenye hili niendelee kukuomba uamini kwamba Tanzania ni rafiki wa kweli kwenye mipango ya Shirika, mafanikio ya kupunguza vifo vya mama na mtoto yanatokana na mahusiano yetu, tunataka tupunguze zaidi na ikiwezekana tuiondoe, inaweza kuwa sio rahisi lakini ishuke chini ya robo,” alisema

Kwa upande wake, Dkt. Githinji aliipongeza Serikali ya Tanzania Serikali kwa kupunguza Vifo vya Mama hadi 104 kwa kila vizazi hai 100,000 ikiwa ni punguzo la asilimia 80 kutoka 2016.

“Hii ni chini ya wastani wa kimataifa wa vifo 211 kwa kila vizazi hai 100,000 na wastani wa kikanda wa vifo 391 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa Kusini na Mashariki mwa Afrika,” alisema Gitahi

Amref imekuwa ikishirikiana na Tanzania kwenye maeneo ya ujenzi wa mifumo ya afya, Kujengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii, magonjwa ya mlipuko, magonjwa ya kifua kikuu, ukimwi na malaria na eneo la afya ya mama na mtoto”

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram