Na Mwandishi wetu WAMACHINGA ZANZIBAR
Yafikisha milioni 85, wamshukuru Rais
KLABU ya Yanga, imeendelea kutembelea upepo mzuri wa kuvuna mamilioni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Yanga juzi usiku visiwani Zanzibar, imewafunga kuwafunga magoli 6-0 timu ya CBE ya nchini Ethiopia, hivyo kupata Sh Milioni 30 za Rais Samia, kama sehemu ya motisha ya ushindi wao aidha timu hiyo ilikabidhiwa Milioni 5 za goli moja walilofunga Ethiopia.
Kwa ushindi huo, Yanga imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/5, ikiwa ni mwendelezo mzuri katika michuano ya Kimataifa kwa Yanga.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Rais wa Yanga, Engineer Hers Said, alisema motisha ya Rais Samia inachangia kwa kiasi kikubwa timu yao kupata mafanikio makubwa katika michuano ya Kimataifa.
Alisema tangu Rais Samia aanze kuonyesha upendo kwa vilabu vya Tanzania, timu yao imekuwa ikitumia mwanya huo kuhakikisha kwamba wanatamba katika michuano ya Kimataifa, wakiamini kuwa goli la mama ni maalum kwa kuwapa wachezaji wao moyo wa kufia uwanjani kama sehemu ya kukuza mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania.
“Upendo huu ni mkubwa kwa Rais wetu, hivyo tunamshukuru mama Samia kwa kutuweka pazuri ndani na nje nchi, ndio maana tunashinda kwa goli nyingi uwanjani kwa sababu wachezaji wanafahamu shauku ya Rais wetu ni kuona timu inashinda na kupata mafanikio makubwa” alisema.
“Hata ukiangalia wachezaji wanapokuwa uwanjani, utagundua nguvu zao nyingi zinachagizwa pia na mamilioni ya Rais Samia, kwetu Yanga tunamshukuru kwa kuonyesha upendo dhidi ya timu yetu,” Aliongeza Said.
Tangu Rais Samia aanzishe motisha ya Goli la Mama, Yanga wameonyesha shauku kubwa ya kupata fedha hizo, ambapo kwa msimu huu tu tayari wamevuna Sh milioni 85 za Goli la Mama.