Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Waziri Mkuu wa zamani Jaji Joseph Warioba, ameipongeza Tume ya Haki Jinai iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema imefanya kazi nzuri katika kwa kufika katika maeneo mengi yenye faida kwa Taifa hususan katika upande wa demokrasia.
Warioba aliyasema hayo jana katika majadiliano ya kidemokrasia yaliyoandaliwa na Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD) akiwa kama mgeni rasmi, huku akisikilizwa na wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo wanasiasa wa vyama mbalimbali vya siasa nchini Tanzania.
Aidha katika kongamano hilo pia Jaji Warioba aligusia umuhimu wa umuhimu wa wadau wote kukaa mezani kuangalia namna nzuri ya kulikwamua Taifa kutoka kwenye mkanganyiko wa kisiasa.