18 views 3 mins 0 comments

PUMA ENERGY YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

In BIASHARA
September 11, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-DAR ES SALAAM

KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, Kampuni ya Puma Energy Tanzania kupitia PumaGas imezindua kampeni ya Bei kama Mkaa tu faida kibao yenye lengo la kuwahimiza wananchi kupika kwa nshati ya gesi.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika jana katika Viwanja vya Zakhem, Mbagala mkoani Dar es Salaam ambapo pia wananchi wameelimishwa kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia hususan ya PumaGas ambayo ni rafiki wa usafi na mazingira.

Akizungumza katika kampeni hiyo Meneja Masoko wa Puma Energy Tanzania, Lilian Kanora alisema kampeni hiyo inalenga kuelimisha jamii na kuhimiza matumizi ya nishati safi kwani PumaGas inaokoa muda wa mama katika kupika, pia inatoa uhakika kwa mama kutoathirika kiafya kwa kuvuta moshi mwingi akiwa jikoni anapika.

Kutokana na hali hatua hiyo, alisema kuwa kupika kwa nishati safi ya PumaGas kunasaidia ulinzi wa mazingira kwani hakutakuwa na sababu ya baba au mama kwenda kukata kuni porini na kuharibu mazingira.



“Nitawapa mfano kopo moja la mkaa ni Sh1000 hadi Sh.2000 na kwa familia inayopika milo mitatu kwa siku hii ni sawa na Sh.2000 hadi Sh.4000 kwa siku.

“Ukipiga hizi hesabu kwa mwezi ni zaidi ya Shilingi 60,000 wakati PugaGas kilo sita ni Shilingi 41,000. Katika kampeni hii kutakuwa na punguzo la bei kwa mtungi wa kilo 15 awali mteja alikuwa akipata gesi na mtungi mpya kwa Shilingi 75,000 ila kwa kipindi hiki kuna punguzo hadi Shiling 66,000.

“Mtungi wa kilo sita utapatikana kwa Shilingi 41,000 tu na mtungi wa kilo 38 pamoja na gesi unapatikana kwa Shilingi 110,000,”alisema na kusisitiza Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeweka mkakati maalum wa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mauzo PumaGas katika Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Jeffrey Nasser aliwaomba wananchi wote kuunga mkono kampeni hiyo huku akishauri hasa wanaume kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa kuwezesha familia kutumia nishati safi ya kupikia ya PumaGas.

“Nitoe rai kwa wanaume ambao ndio baba wa familia,kuna msemo wa baba ni kichwa cha familia basi sasa wanaponunua mahitaji ya nyumbani yakiwemo ya chakula wahakikishe wananunua na nishati safi ya kupikia,” alisema

Akizungumza kuhusu mikakati ya kuhakikisha PumaGas inafika kwa wananchi wengi amesema baada ya kuanza na mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wanaendelea kutanua wigo na siku za karibuni watafikisha huduma ya mitungi ya PumaGas Dodoma na maeneo mengine na kufafanua PumaGas inapatikana kwa mawakala wao pamoja na vituo vya mafuta vya Puma.



Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa Mbagal na Pwani ambao wameshiriki katika uzinduzi wa kampeni hiyo wamesema wanatambua juhudi za Rais Samia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia hivyo nao wanamuunga mkono na wameshaachana na matumizi ya kuni na mkakati

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram