Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Viongozi wa Shirikisho la Umoja wa wafanya biashara ndogondogo (Machinga)kutoka katika Mikoa 20 ya Tanzania bara wamekutana leo 11Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo wamekuwa na maazimio mbalimbali ya kuimarisha umoja wa shirikisho hilo.
Akizungumza katika mkutano huo Uliofanyika JM Hotel Mwenyekiti wa Muda wa shirikisho la Wamachinga Steven Lusinde amesema lengo la mkutano huo nikuweka wazi maazimio ya wamachinga wote nchini ambapo lengo kuu likiwa ni kufanya marekebisho ya rasimu ya katiba ya wamachinga kwa mujibu wa maelekezo ya msaji wa vyama vya kiraia nchini, kuanzisha SACCOS za wamachinga zitakazosajiliwa Nchi nzima na kutatua migogoro baina ya wamachinga na Serikali.
Katika hatua nyingine Lusinde kwa niaba ya wamachinga wote amemshkuru Rais Samia Suhulu kwa kujenga vituo vya biashara vya wamachinga (Machinga Comprex) na kuongeza kuwa wamachinga wanaunga mkono juhudi za serikali za kuleta maendeleo na kwamba wapo tayari kutoa ushirikiano kwa kulipa kodi ili kukuza uchumi.
Akizungumza katika kikao hicho Lusinde amesema kuanzishwa kwa SACCOS hizo kutaweka urahisi kwa wamachinga kupata fursa ya mikopo ambayo inatolewa na Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba imekuwa vigumu kwao kupata mikopo hiyo inayopitia Halmashauri kutokana na kutokuwa na SACCOS na vikundi maalum.
“Tunatamani tuwe na elimu juu ya kitambulisho cha mjasiliamali tujue faida ya kuwa na kitambulisho ili tununue bila kusukumwa”ni ombi lililowasilishwa na mwenyekiti wa shirikisho Steve Lusinde mbele ya waandishi wa habari wakati akizungumza katika kikao cha viongozi wa Machinga 11 Septemba mwaka huu Jijini Dar es Salaam.