ZIARA ya kikazi imefanywa kukagua miradi ya kimaendeleo katika kata ya Pembamnazi iliyopo wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es salaam ikuhusisha maeneo muhimu katika jamii ikiwemo Elimu, Afya na miundombinu
huku ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM )kata Ndg.Muharami Rajabu na Diwani wake Lyona Ramadhani
Ziara hiyo imefanyika Septemba 10.2024 na akiongea wakati anakagua miradi , Mwenyekiti Muharami amesema kwa pekee wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia kwa kuwapendelea kwa miradi elekezi na katika ziara hiyo wameona changamoto ambazo zinawagusa watendaji waliopo na baadhi Serikali hivyo wao kama chama wataenda kutoa tamko ili kipi kifanyike kutatua changamoto hizo
“Tutaenda kufanya tathimini kipi kifanyike ili kuboresha haya maeneo ,Serikali hii tumepokea miradi mingi ukifanya tathmini tumepokea kiasi cha zaidi ya Billioni 200 ,kama kuna sehemu kuna mapungufu tutaielezea Serikali ili fedha zilizotolewa zitumike ipasavyo kwa manufaa ya jamii” Mwenyekiti Muharami
Ameongeza kua katika kiasi cha fedha kilichotolewa kaisi cha Bilioni Mbili au tatu kimeekwa katika kata ya pemba mnazi kwaajili ya maendeleo ya jamii ametaja miradi ni pamoja na Ujenzi wa Daraja kubwa la Sangatini ,Kituo cha afya cha Tundwi ,Mradi wa shule za Sekondari mbili ambapo zipo upande wa Buyuni na Tundwi Songatini na maeneo mengine
Hata hivyo ameainisha Changamoto kwa kuitaja Shule ya Mumba ambayo ilikua shule shikizi na sasa imesajiliwa lakini haina walimu wakutosha ,Ofisi ya Walimu pamoja na Nyumba za walimu
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Pembamnazi Lyoba Ramadhani Yamringa amesema kwa asilimi Tisini miradi imekamilika na inaendelea vizuri hivyo kazi yao kama viongozi ni kuisimamia miradi lakini wapo baadhi ya Walimu wakuu wanatumia fursa hiyo kushikilia miradi na kujifanyia mambo yao binafsi
“Anaetakiwa kuambiwa ameupiga mwingi ni Rais Samia pekee sisi wengine ni watekelezaji tu ,Ukiambiwa umeupiga mwingi tuambie fungu umetoa wapi?, Tunamshukuru Rais kwa fedha lakini ziara imebaini baadhi ya Walimu wakuu wanashikiria miradi na kujichukulia fedha na Miradi ambayo inakasoro tunakwenda kuitolea taarifa “Diwani Lyoba
Amemaliza kwa kusema Matunda ya ziara kata ya pembamnazi ni kua wamegundua tokea uhuru kata hiyo haijawahi kupokea maendeleo kama hayo hivyo matarajio yao ni kumlipa Rais Samia 2025 kwa kura nyingi za kishindo kuanzia Serikali za mitaa madiwani na mpaka yeye mwenyewe
Nae Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mumba ,Mwl Mudhihiri Salum Sasya amesema wamepata Mradi wa chumba kimoja cha Darasa ambao walipokea fedha kiasi Tsh .Milioni 20 Januari mwaka huu kutoka chanzo cha mapato ya ndani na sasa wapo katika hatua za mwisho huku akisisitiza Ziara imempa mwanga kua wanatakiwa watekeleze miradi hiyo ipasavyo na kwa uwazi
Kamati ya siasa iliweza kukabidhi kiasi cha elfu sitini na zaidi kwa Mwalimu huyo fedha ambazo zilichangishwa na Mwenyekiti Muharami Rajabu wakati Shule ilipotangaza inauhitaji wa fedha kwaajili ya marekebisho ya madawati
Ikumbukwe Wametembelea Shule ya Msingi Kichangani,Kituo cha Afya Tundwi Songani ,Shule ya Sekondari Mahenge ,Daraja la Kitomondo na maeneo mengine waliyokagua miradi hiyo
Aidha ,Manispaa ya Kigamboni kwa mwaka wa fedha 2023-2024 ilifanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 17.6 na kuelekezwa katika maeneo kama Afya,Elimu na miundonmbinu.